Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Katoliki washusha waraka ‘Ujumbe wa Kwaresma’
Habari Mchanganyiko

Katoliki washusha waraka ‘Ujumbe wa Kwaresma’

Spread the love

KANISA Katoliki Tanzania limetoa waraka uliobeba ujumbe wa Kwaresima, huku likiangazia changamoto zinazokabili familia na visababishi vya changamoto hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Waraka huo uliotolewa jana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) umeeleza kuwepo kwa dhana potofu na nadharia zisizo sahihi zinazolenga kuhalalisha vitendo vinavyosababisha kutenganishwa kwa ndoa na familia.

Waraka huo umeainisha kuwa, zipo mila na tamaduni ambazo zinachochea uwepo wa changamoto katika familia, ikiwemo tamaduni zinazoruhusu talaka, ndoa za utotoni, uchumba sugu, ndoa za jinsia moja na ndoa baada ya ndoa halali ya kwanza.

“Sisi kama wadhambi tulio safarini kuelekea huo utakatifu, kwa mwaka huu wa 2019 baada ya kuadhimisha miaka 150 ya Kanisa Katoliki Tanzania mwaka jana, tumeona ujumbe wa mwaka huu uzingatie dhamira inayohusu familia zetu,” inaeleza sehemu ya waraka wa TEC.

Familia zenye mchanganyiko wa imani, zinazoishi katika mazingira magumu ya uchumi, familia zisizoishi imani, familia zisizo na maadili, familia zilizopoteza uwezo wa kulea na familia zisizo na kipato, ni changamoto nyingine zilizotajwa katika waraka huo.

“Ili katika kujitafakari na kuamsha upya maisha yetu ya imani Katoliki na maadili yake, tutambue zaidi na tukiri kwa dhati jinsi hali yetu ilivyo mbele ya Mungu ambaye ndiye chanzo cha utakatifu,” TEC inaeleza katika ujumbe wake huo

Waraka huo umebainisha kuwa, kuna harakati zinazopigia upatu uhuru usio wa kweli kwa mwanadamu na kupotosha ukweli kwa kutenganisha ukweli wa maisha na ukweli wa asili katika viumbe na maumbile yao.

TEC inaeleza kuwa kila mwaka hutoa ujumbe mahsusi kwa jamii katika kipindi cha Kwaresima likilenga kuionya jamii ili kuenenda katika njia sahihi.

“Dhamira hii ya familia kama kanisa la nyumbani na shule ya imani na maadili, kwa mwaka huu basi, tutafakari kwa namna gani hili lifanyike kwa kuzingatia kuwa familia ya kikristu ni shule ya imani Katoliki na maadili yake,” ianeleza sehemu ya waraka wa TEC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!