October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makamba: Ningeshangaa Mgeja kubaki Chadema

Spread the love

KUREJEA kwa Hamis Mgeja katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana tarehe 6 Machi 2019, hakukuwashtua wengi. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Mgeja, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga alijiunga Chadema, muda mfupi baada ya swahiba wake Edward Lowassa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kuhamia chama hicho (Chadema) baada ya jina lake kukatwa kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 upitia CCM.

Salome Makamba, Mbunge Viti Maalum wa Chadema mkoani Shinyanga amesema, angemshangaa Mgeja kama angeendelea kubaki ndani ya Chadema wakati Lowassa akiwa tayari amerejea CCM.

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE Makamba amesema,  angeshangaa Mzee Mgeja kubaki Chadema kwa kuwa, inafahamika kwamba alipo Lowassa na mzee huyo yupo.

Ameeeleza kuwa, Mgeja anapaswa kufuta kauli yake kwamba, anastaafu siasa, kauli aliyoitoa miezi michache iliyopita.

 “Mzee Mgeja ni mtu wa Lowassa na alipo Lowassa yeye yupo, ningeshangaa kama angeendelea kuwepo Chadema wakati Lowassa yuko CCM.

“Hatukutegemea kama wazee kama hao (Lowassa na Mgeja) watafaya walichofanya, kwa umri wao tunasema fabililah,” amesema na kuongeza;

“Ukimsikiliza Mzee Mgeja anasema anarudi CCM wakati alitangaza amestaafu siasa lakini anatangaza karudi, kama ameamua kurudi asisahau kuifuta kauli yake kabla hajaendelea na harakati zake sababu si mwanasiasa, alishastaafu siasa.”

error: Content is protected !!