December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Namna Kibonde alivyoanza safari ya kifo chake

Spread the love

SAFARI ya mwisho ya Ephrahim Kibonde, mtangazaji na Mahiri wa  Clouds FM aliyekuwa akitangaza kipindi cha Jahazi,  ilishika kasi siku ya mazishi ya Ruge Mutahaba yaliyofanyika katika Kijiji  cha Kiziru, Bukoba mkoani Kagera. Anaripoti Bupe Mwakiteleko…(endelea).

Akiwa msibani hapo, Kibonde ndiye aliyekuwa mtangazaji wa shughuli za mazishi zilizokuwa zikiendelea na hapo mwisho  wake ulianza kudhihiri.

Mmoja wa watangazaji wa Clouds aliyeomba kutoandikwa jina lake hapa amesema, yapo mambo yaliyotokea kwenye msiba wa Ruge yanayoendana na mwisho wa uhai wake.

Mwandishi huyo anasimulia, Kibonde alianza kujisikia vibaya wakati wa shughuli za mazishi ya mfanyakazi mwenzie,  rafiki yake wa muda mrefu Ruge.

Kibonde alianza kuishiwa nguvu ambapo dada wa marehemu Ruge alimsaidia. Dada huyo pamoja na watu waliokuwepo karibu wakamsaidia kumuingiza ndani na kuanza kumpepea.

Alipoana hali inazidi kuwa mbaya, dada huyo alimwita  Dk.Isack Maro ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Njia Panda na Afya Cheki kwa ajili ya huduma ya kwanza.

Dk.Maro alimpatia huduma ya kwanza na kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera.

Kesho yake (Jumanne) ilibidi wenzake waliokuwa wana ratiba ya kusafiri na ya kurudi Dar es Salaam baada ya kumaliza maziko, walilazimika wamuache Bukoba ili aendelee na matibabu zaidi.

Akiwa anaendelea na matibabu hospitalini hapo, hali yake ilizidi kuwa mbaya, wakafanya uamuzi wa kumuhamishia Hospitali ya Uhuru jijini Mwanza, wakati akipelekwa hospitali ya Bugando leo asubuhi kwa matibabu zaidi umauti ukamkuta.

Taarifa za msiba huo tayari zimedhibitishwa na uongozi wa Clouds Media pamoja na John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa  Mwanza.

“Mtangazaji wa Clouds FM Kibonde amefariki dunia hapa Mwanza, alianza kusumbuliwa na presha alipokuwa Bukoba kwenye msiba wa marehemu Ruge Mutahaba na kuhamishiwa  Mwanza,” amesema Mongella.

 

 

error: Content is protected !!