Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kanisa la Mlima wa Moto watangaza wiki ya maombelezo
Habari Mchanganyiko

Kanisa la Mlima wa Moto watangaza wiki ya maombelezo

Mch. Getrude Lwakatare
Spread the love

MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto lililopo Sabasaba Jijini Dodoma, Slivanus Komba ametangaza maombi ya Maombolezo ya siku saba ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Dk. Getrud Rwakatale. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mchungaji Komba ambaye pia ni Askofu wa Kanda ya Kati na  Nyanda za Juu kusini amesema lengo la maombolezo hayo ni kumuenzi kwa vitendo kutokana na mema na maonyo alikuwa akiyatenda mbeba maono wa Kanisa hilo na aliyekuwa askofu mkuu wa Kanisa la Mlima wa Moto Tanzania, Marehemu Mch. Rwakatale.

Askofu Komba alisema pamoja na kutangaza maombolezo ya siku saba ya Kanisa hilo pia litaendelea na maombolezo ya siku 40 ambayo yametangazwa kitaifa na Kanisa hilo ambayo yatakuwa ya kitaifa.

Kiongozi huyo wa Kiroho alisema kuwa kibiblia hakuna kioongozi yeyoye wa kidini ambaye anaweza kufanya maombolezo kwa ajili ya kumshawishi Mungu kubadilisha mawazo ya mtu aliyekufa kumpeleka peponi au motini kulingana na kile ambacho alikitenda akiwa hai.

Alisema wakati wa uhai wa Mch. Dk. Rwakatale alikuwa ni mstari wa mbele katika kuhakikisha kazi ya Mungu inasonga mbele licha ya kuwa alikuwa mfanyabiashara mkubwa na mwanasiasa.

Katika ibada hiyo ambayo ilikuwa ya tofauti ambayo ilighubikwa na majonzi vilio kwa washirika wa kanisa hilo, Askofu Komba aliwataka waumini wote kuhakikisha wanahudhuria Ibada zote za siku bila kukosa ikiwa ni sehemu ya maombolezo.

Katika hatua nyingine, Askofu Komba amekemea baadhi ya uzushi juu ya wanaopakaza kuhusu mrithi wa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo.

“Pamoja na kuwa Mimi siyo msemaji wa Kanisa hili wapo wasemaji lakini nipende kusema kuwa kwa sasa tupo katika kipindi kigumu cha kuondokewa na Kiongozi wetu mbeba maono.

“Nashangaa kwa mtu yeyote ambaye anawaza kurithi sisi hatupo kwa ajili ya kurithi, tunawaza kufanya kazi ya Mungu na kwa sasa Kanisa lipo ya Baraza la wazee.

“Kwa mtu ambaye anawaza kurithi hana nia njema na huduma ya kuifanya kazi ya Mungu bali maamuzi yote yatatolewa na Baraza la wazee wa kanisa baada ya siku 40,” alisema Askofu Komba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!