Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yaeleza mashaka ya Lissu kurejea
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yaeleza mashaka ya Lissu kurejea

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema
Spread the love
TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), harejei nchini kwa kuwa, bado ana mashaka na maisha yake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kwamba, Jeshi la Polisi halijajibu ombi lake ama kumuhakikishia usalama wake pale ataporejea nchini. Kwa zaidi ya miaka miwili na nusu sasa Lissu yupo nje ya nchi baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana jijini Dodoma tarehe 7 Septemba 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi tarehe 25 Juni 2020, jijini Dar es Salaam John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema amesema, Lissu bado hajahakikishiwa usalama wake na Jeshi la Polisi.

Mnyika amedai, mara kadhaa viongozi wa Chadema wamemuandikia barua IGP Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, kwa ajili ya kuomba ulinzi wa Lissu wakati ataporudi lakini hawajajibiwa.

Amesema, ukimya wa polisi kuhusu usalama wa Lissu, umesababisha mwanasiasa huyo aliyeko ughaibu kutorejea nchini, licha ya kukamilisha matibabu yake.

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, wakati akiwa hospitali

“IGP yeye binafsi hajajibu iwe kwa barua au hadharani tangu tarehe 23 Disemba 2019, nilimuandikia barua rasmi kuomba ulinzi wa polisi kwa ajili ya makamo mwenyekiti ambaye amekuwa akiishi nje ya nchi kwa matibabu tangu Septemba 7 2017,” amesema Mnyika na kuongeza:

“Lissu amekamilisha matibabu yake, na sasa licha ya kuandika barua na kukumbusha Januari 7 mwaka huu bado hujapatia majibu ya ombi letu, kimya chako hakipendezi IGP.”

Lissu kwa sasa yuko nchini Ubelgiji, alikokwenda kufanyiwa matibabu, baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana, akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.

Hata hivyo, Mnyika amesema Chadema inaendelea kushirikiana na Lissu kuangalia namba gani watakavyoshughulikia safari yake ya kurejea nchini.

“Kutojibiwa na IGP haiwezi kuwa kikwazo, sisi kama chama kwa kushirikiana na Lissu tutalishughulikia hili jambo, kwa kuwa IGP amejitokeza mbele ya habari kuzungumzia ujio wa Lissu, aulizwe aeleze kwa nini hajajibu barua ya Mbowe kuhusu Lissu kuhakikishiwa usalama wake,” amesema Mnyika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!