Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema: Siku 60 za kampeni zitafidia miaka 5 ya giza
Habari za Siasa

Chadema: Siku 60 za kampeni zitafidia miaka 5 ya giza

Tundu Lissu, mgombea wa Urais wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeeleo (Chadema), kimesema kitatumia siku 60 za kampeni za uchaguzi kwa kasi kufidia miaka  mitano ya kuwa kigzani katika kujieleza kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).    

Kauli hiyo imetolewa na Halima Mdee, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) jana tarehe 4 Agosti 2020 katika Mkutano Mkuu uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Mdee amesema, viongozi na wanachama wa chama hicho watafanya kazi kama mchwa katika kampeni hizo ili kuhakikisha wanashinda.

“Ili kueleza sera zetu zikoje,  mbadala wetu ukoje ambapo hatujapata nafasi  miaka mitano, tuna  wajibu mkuu na mkubwa wa kuhakikisha siku  60 za kampeni kila mmoja hapa kutoka kwenye eneo lake anafanya kazi kama mchwa,” amesema Mdee.

Halima Mdee

Mdee ameongeza “hawa jamaa ni wepesi kama karatasi, kwa hiyo nawaomba sana hatuna kupumzika leo tunakutana pamoja, tukiondoka kila mmoja akatekeleze wajibu wake.”

Wakati huo huo, Mdee amesema wanawake wa Chadema wamejipanga kuzunguka nchi nzima kufanya kampeni, ili kutafuta ushindi wa chama hicho.

“Wanaume tunawapenda tuko pamoja tuko tayari kupambana,  sasa hivi tunawapima jeshi litaenda kupambana na mademu?  Maana siku zote wanapambana na wanaume, sasa tutaenda kuzunguka kila wilaya na kanda tuone kama Jeshi la Polisi litaenda kupambana na mademu,” amesema Mdee.

Aidha, Mdee amewataka wanaume kuwaunga mkono wanawake waliopitishwa kugombea nafasi za ubunge na udiwani, kwa kuwa wanaweza kuleta ushindi.

“Ushindi wa kura za maoni wa wanawake wa ngazi ya ubunge na udiwani sio kazi ya kubahatisha,  mnajua 2010 tulikuwa tuko watatu tunagombea majimbo nikatawazwa peke yangu, mwaka  2015 mlitupa nafasi tisa tukachomoza sita kupambania majimbo, leo tunataka makamanda mtuunge mkono. Msituletee fitina tuwaunge mkono wanawake wanaoshinda,” amesema Mdee.

1 Comment

  • Ni kipi kipya au cha zaidi ambacho mnataka kutueleza jamani? Kwa sababu yale watanzania walikuwa wanayaota na kuyataka yameshafanywa na mengi yanakuja. Tuwaombe kama hamwezi ku Support kile kinacho onekana kwa macho msituletee fujo na kauli zenu za uongo na kupiga deal kweupe mchana watanzania wamechoka na maneno wanataka maendeleo please please kajipangeni mje huko baadaye sio wakati huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!