Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC kuanza kutoa fomu za urais leo
Habari za Siasa

NEC kuanza kutoa fomu za urais leo

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaanza kutoa fomu za uteuzi kwa wagombea urais wa Tanzania na makamu wake, kuanzia leo Jumatano tarehe 5 -25 Agosti 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya NEC imeeleza, fomu hizo zitatolewa ofisi za tume hiyo Njedengwa jijini Dodoma.

Uteuzi wa nafasi hizo itakuwa tarehe 25 Agosti 2020 ofisi za NEC, Dodoma.

Pia, fomu za uteuzi kwa wagombea ubunge, zitatolewa tarehe 12-25 Agosti 2020 katika ofisi za halmashauri nchini.

Fomu za udiwani zitatolewa tarehe 12-25 Agosti 2020 katika ofisi za kata husika.

Kampeni zitafanyika kuanzia tarehe 26 Agosti 2020 hadi 27 Oktoba 2020 na uchaguzi mkuu utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC)

Tayari vyaka mbalimbali vya siasa nchini vimepitisha wagombea urais ndani ya vyama vyao ili kushiriki uchaguzi huo.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha Rais John Pombe Magufuli na mgombea wake mwenza ni, Samia Suluhu Hassan.

Tundu Lissu, amepitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) huku Salum Mwalimu akipitishwa kama mgombea mwenza.

Wengine ni; John Shibuda wa Ade-Tadea, Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama Cha Wananchi (CUF) na Hashim Rungwe wa Chaumma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!