Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema, ACT-Wazalendo waingia ‘mzigoni’
Habari za SiasaTangulizi

Chadema, ACT-Wazalendo waingia ‘mzigoni’

Spread the love

WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema, kikijifungia leo tarehe 7 Novemba 2019, kikijadili mikiki inayokumbana nayo kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, Chama cha ACT-Wazalendo kimechukua mkondo huo. Anaripoti Martin Kamote … (endelea).

Hatua ya vyama hivyo viwili, kujichimbia kujadili ghiliba zinazofanya na wasimamizi wa uchaguzi huo, ili kukisaidia chama tawala – Chama Cha Mapinduzi (CCM), imelenga kutafutia mwarobaini wake.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Dorothy Temu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo amesema, ushirikiano imara na vyama vingine vya upinzani, unaweza kuondoa kile alichokiita hujuma za CCM.

“Hakuna namna, kinachofanywa kwa sasa si kwa bahati mbaya, wasimamizi wana maelelezo ya CCM ama serikali. Kila chama kikienda kivyaka hakiwezi kufanikiwa, lazima tukabili upuuzi  huu,” amesema.

Ameeleza kuwa, Kamati ya Uongozi ya ACT-Wazalendo itaketi kwa dharura ili kutafakari matukio yanayoendelea kutokea, pamoja na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na matukio hayo.

Wakati chama kikipanga kukutana, John Mrema, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema amesema, Kamati Kuu ya chama hicho inakutana leo kupitia na kutoa uamuzi kulingana na taarifa walizo nazo na namna hujuma zilizofanywa kawa wagombea wao.

“Tumeitisha kikao cha dharura cha kamati kuu na baada ya kikoa hiki tutakutana na wabunge na kisha tutatoa msimamo wa chama,” amesema Mrema.

Temu amesema, ACT-Wazalendo kimefanya mawasiliano na vyama vingine vya upinzani, ili kuunganisha nguvu katika kukabiliana na hujuma hizi zilizofanyika.

“Kamati ya uongozi ya ACT imeitisha kikao cha dharura, kwa ajili ya kutafakari hali hii mbaya ya kisiasa, na kupendekeza hatua za kuchukuwa,  iwapo wanachama wetu hawatarudishwa kugombea,” amesema Temu na kuongeza;

“Huu ni wakati mufaka kwa vyama vya upinzani kuwa na mshikamano dhidi ya udhalimu wa Serikali ya CCM.

“Tumekuwa na muungano tangu tuliposhirikiana kushughulikia sheria ya vyama vya siasa, hujuma kwa chama kimoja ni hujuma kwa chama kingine, tutazidi kuwaita wengine zaidi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!