May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Baada ya Zahera, Yanga wavunja Kamati ya Mashindano

Hassan Bumbuli, Afisa Habari wa Yanga

Spread the love

KAMATI ya Utendaji ya Klabu ya Yanga, imeivunja Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 7 Novemba 2019, na Hassan Bumbuli, Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, kamati hiyo ilivunjwa rasmi tarehe 2 Novemba,  mwaka huu.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, uamuzi wa kamati hiyo kuvunjuwa, ulifikiwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji  kilichoketi katika makao makuu ya klabu ya Yanga Jangwani, jijini Dar es Salaam, chini ya Dk. Mshindo Msolla, Mwenyekiti wa klabu hiyo.

“Uamuzi wa kuivunja kamati ya mashindano, ulifikiwa katika kikao cha kamati ya utendaji kilichoketi Novemba 2, 2019 makao makuu ya klabu, “ inaeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kamati mpya ya mashindano itatangazwa baadae na uongozi wa klabu hiyo.

error: Content is protected !!