Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bodaboda, Bajaji walalamikia polisi, Mambosasa awakana 
Habari Mchanganyiko

Bodaboda, Bajaji walalamikia polisi, Mambosasa awakana 

Spread the love

WAENDESHA Bajaji ambao ni walemavu katika Kituo cha Feri, jijini Dar es Salaam wamelalamikia kitendo cha Jeshi la Polisi kukamatwa wenzao. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wametoa malalamiko hayo ikiwa Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kupiga marufuku kwa bajaji na bodaboda, kuingia katikati ya jiji hadi mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakapomalizika.

Wameeleza, katazo hilo lilitakiwa kukoma jana tarehe 20 Agosti 2019, lakini leo tarehe 21 Agosti 2019, wafanyabiashara hao wameendelea kukamatwa.

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa niaba ya wenzake kwa njia ya simu leo tareje 21 Agosti 2019, Hussein Mosha amedai kuwa, tangu jana kuna baadhi ya madereva wamekamatwa na polisi kwa kosa la kuingia mjini, licha ya katazo hilo kumalizika jana.

“Kwa leo askari alikuja kutoa taarifa kwamba haturuhusiwi kufanya kazi mjini ambapo tipu zetu ni kutoka Feri, Posta hadi Kariakoo. Tumeongea na kiongozi wetu amesema Kamanda Mambosasa hana taarifa za sisi kuzuiwa kufanya kazi baada ya katazo hilo kuisha,” amesema na kuongeza Mosha.

“Lakini baadhi ya madereva wamekamatwa kwa kosa la kuingia mjini wakati katazo hilo limeisha. Tunahisi kuna hujuma kutoka kwa madereva taksi na magari binafsi waliokuwa wanafanyakazi wakati sisi tumesimama. Hawataki tufanye kazi ili wao waendelee.”

MwanaHALISI Online ilimtafuta Kamanda Mambosasa kwa ajili ya ufafanuzi wa malalamiko hayo kwa njia ya simu, ambaye alisema madai hayo si ya kweli.

Kamanda Mambosasa ameeleza kuwa, ni kweli Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya madereva wa bajaji ambao wamekiuka sheria kwa kufanya shughuli zao bila ya leseni.

Kamanda Mambosasa amesema, si kweli kwamba madereva hao wanasumbuliwa ikiwemo kukamatwa kwa sababu ya kuingia mjini baada ya katatzo hilo kumalizika.

“Kilichotokea ni kwamba watu wazima wanawapa walemavu bajaji wazifanyie kazi pasipo kuwakatia leseni. Wanaendesha na kusafirisha abiria pasipo kuwa na leseni huo ni uvunjaji wa sheria,” ameeleza Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema Jeshi la Polisi halitaruhusu mtu yeyote kufanya kazi ya usafirishaji abiria kwa kutumia bajaji pasipo kuwa na leseni.

Aidha, Kamanda Mambosasa amesema, baadhi ya askari waliokamatwa kwa kosa hilo wamepewa dhamana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!