October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge, wastaafu kuondolewa kwenye nyumba za TBA

Spread the love

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA), wameamua kuondoa wadaiwa sugu katika nyumba zao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

TBA wameeleza kuwa, wapangaji hao mpaka sasa wamesababisha hasara ya Sh 1.5 Bil na kwamba, miongoni mwa wadaiwa sugu ni wabunge na wastaafu.

Kwa mujibu wa TBA, pia watawaondoa wastaafu kwa kuwa, wanapomaliza utumishi wa umma, wana uwezo wa kuwa na nyumba zao.

 Akizungumza na wanahabari tarehe 20 Agosti 2019, Kaimu Meneja Wakala wa Majengo Mkoa wa Dodoma, Helman Tanguye baada ya kufanya zoezi hilo amesema, wadaiwa hao wamelimbikiza madeni yao kwa miaka 10 sasa.

 Amesema, TBA imekuwa ikidai fedha nyingi na hasa katika Mkoa wa Dodoma kwa wafanyakazi wa serikali na taasisi mbalimbali za serikali ambazo wamezipangisha.

“Mpaka sasa tunadai zaidi ya bil 1.5, hivyo lengo kuu la TBA ni kuwaondoa wale watu walioshindwa kulipa kodi ya pango kwa wakati ili watu wanaohamia kutoka mikoa ya Dar es salaam na maeneo mengine, waweza kupata nafasi ya kupanga katika nyumba hizo,” amesema Tanguye.

Akizungumzia zoezi zima walivyolianza amesema, “tumelianza jana baada ya kufanya taratibu zote za kisheria na mikataba, kwa hiyo tuliwapa notes ya siku 30 badaye tukaongeza Siku 14 lakini zilivyokwisha, tulichukua vyombo ambavyo vinatambulika na mahakama ili tuweze kuwaondoa.”

Amesema, kampuni wanayoitumia katika zoezi zima la kuwatolea watu vitu vyao nje ni Yono Auction Mart ambayo wamekuwa wakiitumia mara kwa mara katika shughuli zao.

error: Content is protected !!