Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo Bingwa wa bao la mkono afariki Dunia
Michezo

Bingwa wa bao la mkono afariki Dunia

Spread the love

DIEGO Maradona mchezaji wa zamani na kocha wa Timu ya Taif ya Argentina amefariki Dunia siku chache baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa alipokuwa anasumbuliwa na tatizo la damu kuvilia kwenye Ubongo. Anaripoti Kelvin Mwaipingu, Dar es Salaam … (endelea).

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona na Napoli ya Itaria, alijizolewa umaarufu mkubwa mara baada ya kufunga bao la mkono kwenye mchezo wa robo fainali wa kombe la Dunia dhidi ya Uingereza.

Bao hilo la mkono liliwezesha Argentina kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika nchini Mexico mwaka 1986.

Mwezi Novemba 2020, fundi huyo wa mpira wa miguu alikimbikwa hospitalini baada ya kuugua ghafla na baadae kufanyiwa upasuaji wa kichwa na kufanikiwa kurudi nyumbani kwake huku vyanzo vya taarifa vikieleza Maradona alipoteza maisha baada ya kupata shambulio la Moyo (Cardiac Arrest) akiwa na umri wa miaka 60.

Maradona alifanikiwa kuiingoza timu ya Taifa ya Argentina kwenye fainali nne za kombe la Dunia na kufunga jumla ya mabao 34 katika michezo 90 aliyocheza.

Mwaka 2008 alichaguliwa kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Argentina na kuingoza kwenye fainali za kombe la Dunia 2010 zilizofanyika Afrika Kusini lakini alitimuliwa mara baada ya timu hiyo kutolewa kwenye hatua ya Robo Fainal na Ujerumani.

1991 Maradona alifungiwa miezi 15 kutocheza mpira mara baada ya kupimwa na kukutwa anatumia dawa za kulevya aina ya Cocain.

Fundi huyo wa mpira alitundika daluga 1997 ndani ya Ligi ya Argentina akiwa na umri wa miaka 37 kwenye moja ya miamba ya soka nchini himo klabu ya Boca Junior.

Mpaka umauti unamkuta katika maisha yake kama kocha Maradona pia alifanikiwa kufundisha soka kwenye nchi za Umoja wa falme za kiarabu pamoja na Mexico.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!