December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaipiga Azam FC, yaongoza Ligi

Spread the love

BAADA ya kufanikiwa kuondoka na pointi tatu dhidi ya Azam FC kwa bao 1-0, Yanga sasa inapanda mpaka nafasi ya kwanza, baada ya kufikisha pointi 28 huku Azam Fc ikishika nafasi ya pili ikiwa ikiwa na pointi 25 na Simba ikiwa kwenye nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23 ikiwa na mchezo mmoja mkononi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo lilifungwa na Deusi Kaseke dakika ya 48 mara baada kupokea pasi kutoka kwa Yacouba Sogne kutoka upande wa kushoto wa Uwanja kwenye mchezo uliochezwa  kwenye dimba wa Azam Complex Chamazi.

Kabla ya mchezo huo Yanga na Azam FC zote zilikuwa zinalingana pointi, kila timu kuwa na pointi 25 baada ya kucheza michezo 11 ila Azam Fc alikuwa kujuu kwa tofauti ya mabao ya kufumga na kufungwa.

Katika mchezo huo kocha wa Yanga Cedric Kaze alifanya mabadiliko ya wachezaji watatu katika kikosi cha kwanza ukilinganisha na kile kilichoanza kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo na kufanikiwa kumiliki mpira kwa sehemu kubwa ndani ya dakika 90 za mchezo.

Ditram Nchimbi, Deus Kaseke na Yacouba Sogne yalikuwa maingizo mapya kwenye mchezo huo huku wakichukua nafasi za Carlos Carlinhos, Farid Mussa na Michael Sarpong.

Kwenye mchezo huo Azam Fc ilionekana kupoteza makali yake kwenye eneo la ushambuliaji mara baada ya kuumia Prince Dube 24′ na kutolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Richard Djodi.

Kwa matokeo hayo Azam FC atakuwa anapoteza mchezo wake wa pili mfululizo baada ya kufungwa na KMC kwa bao 1-0 kwenye mchezo uliopita uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!