Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo Amunike awatimua wachezaji wa Simba Taifa Stars
MichezoTangulizi

Amunike awatimua wachezaji wa Simba Taifa Stars

Spread the love

KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars,’ Emmanuel Amunike amewaondoa wachezaji sita wa klabu ya Simba waliokuwa wameitwa kwenye timu hiyo kutokana na sababu za kuchelewa kuripoti kambini kwa wakati ili kujiandaa na mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Wachezaji hao ambao ni John Bocco, Shiza Kichuya, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Shomari Kapombe pamoja na Hassan Dilunga.

Wote hao walitakiwa kuripoti kambini jana ili kuanza maandalizi lakini mchezaji pekee aliyeripoti kwa wakati kutoka ndani ya klabu hiyo ni mlinda mlango Aishi Manura.

Chanzo cha taarifa kutoka ndani ya shirikisho la mpira wa miguu nchini ‘TFF’ zinasema kocha mkuu wa Taifa Stars hakupendezewa na jinsi wachezaji wa timunya Taifa wanavyojivuta kuripoti kambini hivyo kuonekana kuwa ni utovu wa nidhamu.

Wachezaji waliochaguliwa kuziba nafasi hizo ni Salum Kimenya (Prison), Paul Ngarena na Ally Abdukaidir (Lipuli FC) wengine ni Kelvin Sabato na Salum Kihimbwa kutoka Mtibwa pamoja na Frank Domayo na David Mwantika wa Azam FC.

Amunike ataiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza toka aliposaini kandarasi ya kukinoa kikosi hiko, katika mchezo utakao fanyika tarehe 8, Septemba 2018 dhidi ya Uganga katika dimba la Nelson Mandera uliopo Nambole.

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!