January 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo wamlilia Askofu Banzi

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimetuma salamu za pole kufuatia kifo cha Askofu wa Jimbo la Katoliki Tanga, Anthony Banzi. Anaripoti Mwandishi wetu… (endelea).

Askofu Banzi amefariki leo tarehe 20 Disemba 2020, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) alipokiwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.

Taarifa za kifo cha Askofu Banzi zilitolewa na Padre Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza Katoliki la Maaskofu Tanzania (TEC) mapema leo asubuhi na kueleza kuwa tarehe ya mazishi itatolewa baadaye.

“Baraza la Maaskofu Tanzania linasikitika kutangaza kifo cha Baba Askofu Anthony Banzi wa Jimbo la Katoliki Tanga, amefariki leo tarehe 20 Disemba 2020 na tarehe ya mazishi tutajulishwa baadaye,” ilieleza taarifa hiyo.

Kufuatia kifo hicho, Chama cha ACT-Wazalendo kimetuma salamu zake za rambirambi kupitia kwa Janeth Rithe, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano kwa Umma wa chama hicho na kimeeleza kusikitishwa na taarifa hizo za kifo.

Amesema, chama hicho kinatoa pole kwa familia ya Askofu, ndugu na jamaa na kuwataka kuwa na subira katika wakati huu wa msima.

“Chama cha ACT-Wazalendo kimehuzunishwa na taarifa ya kifo cha Baba Askofu Anthony Banzi wa Jimbo la Katoliki la Tanga kilichotokea leo tarehe 20 Disemba 2020 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Katika uhai wake, Baba Askofu Banzi amelitumikia Taifa kiroho kwa upendo mkubwa. Chama cha ACT-Wazaleno kinatuma salamu za pole kwa kanisa la Katoliki Jimbo la Tanga, kwa wakatoliki wote na watu wote walioguswa kwa namna moja ama nyingine, Mungu awape faraha katika kipindi hichi kigumu,” imeeleza taarifa hizo.

error: Content is protected !!