May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yamwalika Rais Samia Uwanjani, mchezo dhidi ya Kmc

Spread the love

KLABU ya soka ya Yanga, imemualika Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan, kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kmc. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo namba 144, utapigwa Jumamosi ya tarehe 19 Machi 2022, majira ya saa 1 usiku, ambayo itakuwa siku ya maadhimisho yam waka mmoja wa Rais Samia tangu aingia madarakani.

Rais Samia ambaye aliapishwa tarehe 19 Machi 2021, kufuatia kuaga dunia kwa mtangulizi wake Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli ambaye alifariki Dunia tarehe 17 Machi 2021.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo tarehe 16 machi, 2022 kwenye makaoamakuu ya klabu hiyo, msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara alisema kuwa, kama klabu ya Yanga lazima waadhimishe mawak ammoja wa utawala wa kiongozi huyo kwa kuwa amefanya vitu vingi katika sekta ya michezo.

“Jumamosi tumemuomba Mama yetu Samia kupitia wizara ya Habari na TFF, ikimpendeza aungane na watanzania wapenda mpira pale uwanjani aje kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wetu dhidi ya KMC.” Alisema Haji

Yanga wanakwenda kwenye mchezo huo huku wakiwa vinara wa Ligi hiyo, mara baada ya kucheza micherzo 17 bila kupoteza.

Aidha Manara aliendelea kusema kuwa, kama ratiba ya mheshimiwa Rais ikiwa vizuri basi atajumuika na jamii ya wapenda mpira Uwanjani hapo.

“Kama ratiba yake Mheshimiwa Rais ikiwa vizuri, tunamini anaweza kuja kujumuika na watanzania katika kusherehekea mwaka mmoja wa uongzoi wake.” Alisisitiza msemaji

Mchezo huo hapo awali ulipangwa kupigwa hii leo tarehe 16 Machi 2022, majira ya saa 1 usiku, lakini ulisogezwa mbele na bodi ya Ligi ili kupisha matengenezo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mkapa.

error: Content is protected !!