WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, amewataka wasanii ambao bado hawajachukua fedha za mirabaha yao, wakamilishe taratibu katika Chama cha Hakimili Tanzania, ili wapate haki yao. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Mchengerwa ametoa wito huo leo Jumatano, tarehe 16 Machi 2022, akitaja mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
“Tunayo orodha ndefu ya wasanii ambao wanapaswa kwenda kupata haki yao na ambao ni wanufaika katika eneo hili. Nichukue fursa hii kuwaomba ambao bado hawajakwenda kuchukua kiasi chao cha fedha waweze kufika COSOTA, kwa ajili ya kukamilisha taratibu na kupokea eneo la mirabaha yao,” amesema Mchengerwa.
Mchengerwa amesema, kiasi cha Sh. 312 milioni, zilikusanywa kama mirahaba ya wasanii, katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2021, ambazo ziligawiwa kwa wasanii 1,123, ambao kazi zao 5,924 zilifuzu vigezo vya kupata mirabaha.
Amesema orodha yote ya wasanii waliokidhi kupata mirabaha hiyo,itatolewa na COSOTA hivi karibuni.
Leave a comment