Saturday , 4 May 2024
Home Kitengo Biashara Wateja wa TotalEnergies kurudishiwa 10% kupitiaushirikiano na LIPA KWA M-PESA
Biashara

Wateja wa TotalEnergies kurudishiwa 10% kupitiaushirikiano na LIPA KWA M-PESA

Spread the love

KUPITIA dhamira yakuendeleza mfumo wa maisha wa kutotumia pesataslimu nchini, huduma ya M-Pesa ya Vodacom naTotalEnergies Marketing Tanzania Limited wamezinduaushirikiano wa kimkakati ili kuwawezesha watejakufanya malipo bila ya kutumia pesa taslimu kwausalama na urahisi katika vituo vyote vya kutoleahuduma vya TotalEnergies. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kupitia ushirikiano huu mpya, wateja watafurahia faidatofauti ikiwemo kurudishiwa 10% ya pesawatakapolipia kwa kutumia M-Pesa kwa siku 15 zijazo. Ofa hii itaendelea mbele zaidi kwa kila Jumamosi kwamiezi mitatu ijayo. Zaidi ya hapo, kupitia ushirikiano huu, pia wateja watapata huduma ya M-Pesa kwashughuli za kibiashara ikiwamo kuweka, kutoa, nakutuma pesa wakiwa katika katika vituo vya kutoleahuduma vya TotalEnergies.      

Ushirikiano wa TotalEnergies na huduma ya M-Pesa yaVodacom umekuja katika muda muafaka, sio kuwapaWatanzania njia rahisi na ya uhakika ya kutumia pesabali pia kuunga mkono jitihada za kidigitali za serikalihususani kuchochea mabadiliko kuelekea kwenyeuchumi wa kidigitali ambapo bado matumizi ya pesataslimu yanaendelea kutumika na kukubalika maeneomengi nchini kote.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huuuliofanyika katika kituo cha kutolea huduma cha TotalEnergies kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania PLC, Bi. Harriet Lwakatare amesisitiza namnaambavyo kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbelekwenye kuunga mkono ajenda ya Tanzania ya kidigitalina kuwa ushirikiano huu mpya ni hatua mojawapokuelekea njia sahihi.  

Tunaendelea kujikita katika kutoa ubunifu waufumbuzi wa kidigitali kuhakikisha tunasaidiamamilioni ya Watanzania kujiunga na kushiriki katikauchumi wa kidigitali. hili linathibitishwa kwa ubunifutunaoendelea kuufanya katika kuunga mkono ajenda yakutotumia pesa taslimu ambapo M-Pesa ina mchangomuhimu ambapo tumeleta mapinduzi ya namnatunavyofanya malipo.

“Ushirikiano huu utasaidia watejawa TotalEnergies kulipia kwa urahisi kupitia M-Pesakwa kufuata hatua chache kwenye simu zao za mkononina kupata huduma mbalimbali kwa urahisi na usalamawa miamala yao wakiwa katika vituo vya kutoleahuduma vya TotalEnergies,” alisema Lwakatare.

Kwa upande wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, Meneja Masoko, Caroline Kakwezi ameelezeakuwa, “TotalEnergies imevutiwa na jitihada za Vodacom kuunga mkono kasi ya utekelezaji wadhamira ya serikali ya kutumia mifumo ya kidigitalikwenye kuleta uchumi jumuishi Tanzania kupitia M-Pesa.

“Ushirikiano huu kati ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited na huduma ya M-Pesa ya Vodacomunaendelea kuchochea zaidi juhudi hizi kwakuwawezesha wateja kulipia mafuta kupitia Lipa Kwa Simu na kupata huduma za M-Pesa za kuweka na kutoapesa. Ushirikiano huu mpya unalenga kuwajengea haliya kujiamini katika matumizi ya majukwaa ya kifedhaya kidigitali kwa kupunguza hatari na mzigounaosababishwa na kutembea na pesa taslimu. Kwa pamoja, Vodacom na TotalEnergies tutaendelea kujizatiti kutoa huduma bora kwa wateja.  

Miaka 10 iliyopita na zaidi, Tanzania imeshuhudiamwamko mkubwa wa matumizi ya huduma za pesakwa njia ya simu za mkononi kama vile M-Pesaambayo inaoongoza njia kwa upande wa malipo yakidigitali. ikiwa na wateja zaidi ya milioni 10 nawafanyabiashara zaidi ya 180,000 kwenye mtandao wake wakitoa huduma ya LIPA KWA M-Pesa nasuluhisho kwa huduma za wafanyabiashara, M-Pesainaendelea kuwa kinara kupitia ubunifu wa ufumbuziwa malipo ya kidigitali ambayo yanaleta urahisi, ufanisina hatimaye kuchochea ujumuishi wa huduma za kifedha kwa Watanzania wote.

Kwa kuongezea, kampuni hizi mbili zinaamini kuwasafari ya kuelekea katika uchumi usiotegemea matumiziya pesa taslimu ni suala ambalo linaweza kufikiwa na nihatua muhimu kwenye uchumi wa Tanzania nazinatumaini kuwa ushirikiano huu utakuwa na mchangochanya kwa maisha ya Watanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cash Days Promo mamilioni yanakusubiri, cheza kupitia Meridianbet kasino 

Spread the love  JIANDAE kwa mshangao wa kustaajabisha Meridianbet kasino ya mtandaoni...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!