Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanawake waislamu waomba msaada ujenzi makao makuu, Bihimba atoa matofali 1,000
Habari Mchanganyiko

Wanawake waislamu waomba msaada ujenzi makao makuu, Bihimba atoa matofali 1,000

Spread the love

BARAZA Kuu la Wanawake wa Kiislamu Tanzania, limewaomba wadau kuchangia ujenzi wa makao makuu yake yaliyopo maeneo ya Kivule, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Ombi hilo limetolewa leo tarehe 16 Septemba 2023, katika harambee ya kuchangisha fedha na vifaa vya ujenzi wa jengo la makao makuu ya baraza hilo, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika harambee hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa baraza hilo, Mayasa Sadala, alisema ili wamepanga kujenga jengo lenye ghorofa tano, lakini wamekwama kutokana na ukata wa fedha.

“Kuna eneo tumepanga kulinunua lakini hatujamaliza fedha tumelipa milioni 40, bado milioni 10 hivyo tunaomba wadau watuunge mkono kumaliza pamoja na kupata fedha za ujenzi wa makao makuu yetu,” ameswma Sadala.

Katika Harambe hiyo, wadau mbalimbali walitoa michango Yao kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa eneo la mikutano unagharimu Sh. milioni sita.

Miongoni mwa wadau hao ni mwanajamii Bihimba Mpaya, aliyetoa matofali 1,000 yanayogharimu zaidi ya Sh. milioni moja na mabati matatu.

“Katibu wenu alinipa mualiko wa kuhudhuria harambee, nilikubali japokuwa sina kitu lakini Mungu amenipa nguvu na sina mali nyingi bali nina moyo wa kutoa. Leo nimekuja na sadala yangu tofsli 1,000,” amesema Mpaya na kuongeza:

“Na mimi sitoi misaada kwa waislamu wenzangu tu bali kwa jamii nzima sababu napenda maendeleo ya watu.”

Akizungumzia mchango huo, Sadala amesema utasaidia kumalizia ujenzi wa sehemu hiyo.

“Tunashukuru Mungu tumepokea tofsli kutoka kwa Bihimba, tunamshukuru sana kwa msaada huu kwa kuwa utasaidia kuendelea harakati za wanawake wa Kiislamu Kivule. Mungu ambariki aendelee kuchangia na tunawakaribisha wengine waweze kuchangia,” amesema Sadala.

Kwa upande wake Amirati wa Wilaya ya Temeke, Sumaiya Abdallah, amewashukuru wadau wote waliotoa michango Yao.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shuraa ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda, amewataka wanachama wa baraza hilo kujenga desturi ya kukutana mara kwa mara kwa ajili ya kuangalia namna ya kuendelea taasisi yao.

“Kama watu hamiutani hamuwezi kufanya kitu, ili watu waweze kuoiga hatua lazima wasaidiane wanakaa pamoja wanajua mambo muhimu wanayopaswa kuyafanya,” amesema Sheikh Ponda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!