Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Askari wa kike Tanzania washiriki Mkutano wa Mwaka 2023 New Zealand
Habari Mchanganyiko

Askari wa kike Tanzania washiriki Mkutano wa Mwaka 2023 New Zealand

Spread the love

 

ASKARI wa Kike kutoka Nchini Tanzania wameshiriki Mkutano wa mwaka 2023 wa Mtandao wa Polisi Wanawake Duniani (IAWP) Nchini New Zealand. Anaripoti Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi, Auckland New Zealand … (endelea).

Mkutano huo umebeba kaulimbiu isemayo” Refresh, Renew,Refocus umefunguliwa September 17,2023 mji wa Auckland.

Aidha Mkutano huo umeudhuriwa na mataifa kama vile Tanzania,Ghana na Africa Kusini.

Itakumbukwa mwishoni mwa mwezi Julai Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano kama huo kwa ukanda ya Afrika uliyofanyika jijini Dar es salaam na kuleta matokeo makubwa ya kiutendaji kwa maafisa na askari wa kike ambao walishiriki na mada mbalimbali kufundishwa lengo likiwa kuwaongezea uwezo na maarifa ya kiutendaji.

Mkutano huo uliofunguliwa leo septemba 17,2023 katika mji Auckland Nchini New zealand unaoambatana na mafunzo ya kuwajengea uwezo askari wa kike, sambamba na kutoa fursa na kutengeneza mtandao wa mawasiliano kwa wasimamizi wa sheria.

Mbali na hilo Ujumbe huo kutoka Tanzania uliongozwa na Kamishna wa Polisi CP Suzan Kaganda wa kamisheni ya Utawala na rasilimali watu umetumia mkutano huo kutangaza utalii na vivutio vya kitamaduni vilivyopo Tanzania.

Mkutano huo hutahitimishwa Septemba 21,Mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Makamba: China ni ya mfani kwa kupunguza umaskini

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, January...

error: Content is protected !!