August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanawake Babati walalamikia kuswekwa Rumande

Spread the love

WANAWAKE wanaofanya biashara ya kuuza samaki  maeneo ya  stendi  kuu ya mabasi mjini hapa wameilalamikia Halmashauri ya Mji wa Babati kuwaondoa  kwa nguvu na kuwasweka rumande bila kuwaandalia mazingira mengine, anaandika Mwandishi Wetu.

Malalamiko hayo waliyatoa wakati wakizungumza na wakiwa  maeneo ya  zima moto  ilipo ofisi ya kata walipokuwa wameswekwa rumande ya kata kabla ya kuwafikisha kituo cha polisi cha Babati.

“Sisi tuna uwezo mdogo wa kifedha na mitaji yetu haizidi  Sh 20,000 wakituondoa hapa tutaenda wapi maana kule wanakolazimisha tuende  hamna wateja  kwa kua sisi tunawauzia wasafiri,’’alisema Janeth Edison.

Wachuuzi hao walisema wanashindwa kukubaliana na  matakwa ya Halmashauri kwa kuwa  eneo wanaloambiwa kupewa sokoni ni nyuma sana ambako hawawezi kupata wateja.

Aidha,  wanasema baadhi ya watumishi wa Halmashauri wamewageuza kitega uchumi chao kwa kua wanawatoza faini  ya Sh 90,000 lakini wakati wakiandika risiti wanaandika wamelipia 50000 suala ambalo walidai linawaumiza.

“Tulipoenda kwa Kaimu Mkurugenzi, Bashir  Mhoja, alituambia  hawatatutafutia eneo jingine  tulipomfuata ofisini  badala yake alisema watatukamata na kututoza faini  au kutufikisha mahakamani,’’ alisema Zakia  Amani.

Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Babati Mjini, Fauswali  Hamadi, alisema  ni vizuri tatizo hilo likamalizwa kwa busara.

Alisema Rais John Magufuli alishatangaza mara kwa mara kwamba wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) waachwe wakiendelea na bishashara zao.

error: Content is protected !!