Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wahitimu NCT watakiwa kuleta mageuzi kwa watalii
Habari Mchanganyiko

Wahitimu NCT watakiwa kuleta mageuzi kwa watalii

Spread the love

Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)  wametakiwa kuleta mageuzi katika utoaji huduma bora kwa watalii na wageni wanaotembelea hifadhi na vivutio mbalimbali ili kuitangaza vyema Tanzania na kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 12 Desemba 2023  na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki kwenye mahafali ya 21 ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika katika Ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam.

”Ninyi ambao mmepikwa katika chuo bora cha utalii na ukarimu nchini nategemea mkalete mageuzi katika huduma mtakazotoa kwa watalii na wageni kwa ujumla, ili watalii na wageni wanaotembelea nchini wapate huduma kulingana na thamani ya fedha yao na pia washawishike kurejea nchini na kuitangaza Tanzania kwa ndugu na jamaa zao,” amesema Kairuki.

Amewaasa wahitimu hao 483 waliotunukiwa vyeti katika ngazi za astashahada na stashahada kwenye fani za ukarimu, utalii na uratibu wa matukio, kutumia vyema ujuzi walioupata ili kupunguza malalamiko katika eneo la utoaji wa huduma bora kwa wageni.

Amesema kwa kufanya hivyo watakuwa wamewezesha na kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika pato la Taifa sambamba na kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuitangaza Tanzania Kimataifa na kushawishi ongezeko kubwa la watalii kupitia Programu ya”Tanzania- the Royal Tour”.

Aidha, amewasihi wahitimu hao kujiendeleza kielimu na kiujuzi ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia kwani sekta ya utalii na ukarimu inakua kwa kasi sana.

Aidha, Kairuki ametoa wito kwa wadau wa sekta ya utalii nchini kutumia huduma za chuo hicho ili kuendelea kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na chuo lakini pia kukiwezesha kuongeza mapato yake ya ndani ili kuendelea kuboresha na kuimarisha mafunzo ya nadharia na vitendo kwa kukidhi gharama za uendeshaji wa mafunzo hayo.

Mahafali hayo yamehudhuriwa na viongozi na Watendaji wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Mabalozi na wawakilishi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa Taasisi mbalimbali kutoka Sekta ya Umma na Binafsi, Watumishi na Wanachuo.

Naye, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dk. Florian Mtey amesema kuwa chuo hicho ni miongoni mwa vyuo vilivyo mstari wa mbele katika kutimiza ndoto ya Serikali ya kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni 5 ifikapo 2025 na pia kuongeza idadi ya watoa huduma wenye ujuzi na weledi stahiki inatimia.

Amewapongeza wahitimu wa chuo hicho kwa kutimiza vigezo vya kutunukuwa Stashahada na Astashahada katika fani na ngazi mbalimbali za uhitimu.

Chuo cha Taifa cha Utalii ni wakala ulio chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wenye dhamana ya kutoa mafunzo,  kutoa huduma ya Ushauri  na kufanya tafiti katika fani ya ukarimu na utalii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!