Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wadau wataka ushirikishwaji kamati kufumua vyombo vya dola
Habari za SiasaTangulizi

Wadau wataka ushirikishwaji kamati kufumua vyombo vya dola

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, ameshauriwa kushirikisha wadau katika uundaji wa kamati ya kushauri namna bora ya ufumuaji wa vyombo vya haki jinai nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo ulitolewa jana tarehe 20 Julai 2022, muda mfupi baada ya Rais Samia kusema ameunda kamati ya wajumbe 12 na sekretarieti yenye watu watano ikiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Chande Othman, kwa ajili ya kumshauri namna ya kuleta mabadiliko ya utendaji wa vyombo hivyo, vikiongozwa na Jeshi la Polisi.

Msemaji wa Sekta ya Mambo ya Ndani wa ACT-Wazalendo, Maharagande Mbarala, amesema kamati hiyo ni vyema ikashirikisha wadau wanaoguswa na huduma ya Jeshi la Polisi, ili kuleta matokeo chanya.

“Uamuzi wa Rais kuunda tume ya wastaafu wenye kushauri mageuzi ya Jeshi la Polisi ni muhimu iwe shirikishi zaidi, kwa kuwahusisha wadau wote wanaoguswa na huduma ya Jeshi la Polisi. ACT Wazalendo tunatoa wito kwa Rais Samia kuongeza wigo wa tume hiyo kwa kuhusisha wadau wengine ili kulifanya Jeshi la Polisi kuakisi matarajio na matamanio ya watanzania wanaowahudumia,” amesema Maharagande.

Naye Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa Chama cha Wananchi (CUF), Mhandisi Mohamed Ngulangwa, alipongeza hatua hiyo huku akitoa wito ukaguzi wa kina ufanyike kwa Jeshi la Polisi.

“Pamoja na pongezi kwa Rais, tunaendelea kutoa wito wa kulifanyia ukaguzi wa kina jeshi hili kwa ngazi zote ili hatimae kuhakikisha tunakuwa na jeshi bora. Matokeo ya ukaguzi huo yatumike kuboresha ufanisi, kudhibiti watumishi waovu, lakini pia kuboresha maslahi na mazingira ya kazi ya jeshi hilo,” alisema Mhandisi Ngulangwa na kuongeza:

“Tunautakia uongozi mpya wa jeshi la polisi utendaji uliotukuka unaozingatia weledi, uwajibikaji na unaoheshimu misingi ya haki za binadamu na utawala bora.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!