November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Vigogo watatu wa soka Afrika, watanguliza mguu moja Qatar

Sadio Mane akiwa kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa ya Senegal

Spread the love

 

VIGOGO wa watatu wa soka Barani Afrika, tayari wamefanikiwa kufuzu kwa hatua inayofuata ya michuano ya kufuzu fainali za kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Qatar Juni, 2022. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Timu hizo ambao ni Mali, Senegal na Morocco wamefanikiwa kuwa vinara kwenye makundi yao, licha ya kusalia kwa mchezo mmoja kwa kila timu ambao utakuwa wa kukamilisha ratiba.

Kwa upande wa Mali wao wamefanikiwa kuwa kinara kwenye kundi E, wakiwa na pointi 13 mara baada ya kucheza michezo mitano huku nafasi ya pili ikishikwa na Uganda wakiwa na pointi 9, ambao hata wakishinda mchezo wao wa mwisho hawataweza kufikia hizo alama,

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Mali

Kwenye kundi H, Timu ya Taifa ya Senegal imeibuka kuwa kinara licha ya kusalia na mchezo mmoja mara baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 13, katika michezo mitano huku akifuatiwa na timu ya Taifa ya wenye alama tano.

Morocco kwa upande wao wamefanikiwa kufuzu mapema, mara baada ya kucheza michezo minne na kujikusanyia jumla ya pointi 12, huku akisalia na michezo miwili mkononi, na kwenye nafasi ya pili ikishikwa na Guinea Bissau wenye pointi nne, ambao hata wakishinda michezo yao mwisho hawatoweza kufikia pointi hizo.

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Morocco

Vigogo hao watatu watasubiri kuungana na timu nyingine saba, na kukamilisha idadi ya timu 10 zitakazofuzu hatua ya mtoano kwa kucheza michezo miwili, nyumbani na ugenini na kisha kupata timu tano zitakazowakilisha bara la Afrika kwenye michuano hiyo mikubwa Ulimwenguni.

error: Content is protected !!