November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Stars kuifuata Madagascar na Ndege ya kukodi

Spread the love

 

TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itaondoka jioni ya leo tarehe 12, Novemba 2021 kuelekea jijini Antananarivo, Madagascar kwa ajili ya mchezo wa mwisho kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia Qatar 2022. Anaripoti Kelvin Mwaipungu….(endelea)

Mchezo huo wa kukamilisha ratiba utapigwa Jumapili ya tarehe 14, Novemba, 2021 huku timu zote mbili zikiwa hazina nafasi ya kusonga mbele kutokana na msimamo ulivyo kwenye kundi J.

Stars inasafiri hii leo kupitia Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, kwa kutumia ndege ya kukodi ya Shirikika la Ndege la Air Tanzania.

Timu hiyo inakwenda nchini Mdagascar huku ikiwa na kumbukumbu ya kichapo cha mabao 3-0, kutoka kwa timu ya Taifa ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, mchezo uliochezwa jana tarehe 11 Novemba 2021 kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Msafara wa Taifa Stars utakuwa na wachezaji 27, ambao waliingia kambini toka tarehe 4, Novemba Mwaka huu kwa ajili ya kujiandaa na michezo hii miwili ya mwisho chini ya kocha Mkuu Kim Poulsen.

Matumaini ya Stars kufuzu hatua inayofuata yalizimwa rasmi jana, mara baada ya Benin kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, wakiwa nyumbani dhidi ya Madagascar na kufanya kufikisha pointi 10, huku wakisalia na mchezo mmoja.

Msimamo wa kundi J, mpaka sasa Benin wapo kileleni wakiwa na pointi 10, waklifuatiwa na timu ya Taifa ya Congo wakiwa na pointi 8, huku Taifa Stars ikishika nafasi ya tatu ikiwa na alama 7, na Madagacsar wakibuluza mkia wakiwa na pointi tatu.

error: Content is protected !!