Tuesday , 30 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Uhuru wa kujieleza umeporomoka’ 
Habari za Siasa

‘Uhuru wa kujieleza umeporomoka’ 

Spread the love

RIPOTI ya Shirika la Utafiti la Afrika Mashariki la Twaweza, inaonesha kwamba uhuru wa watu kujieleza, umeporomoka katika nchi za ukanda huo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa matokeo ya ripoti hiyo iliyotolewa leo tarehe 2 Novemba 2019 Aidan Eyakuze, Mkurugenzi wa Twaweza, imeonesha idadi ya wananchi waliohuru kujieleza katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, imeporomoka.

Nchini Tanzania, uhuru wa kujieleza umeporomoka kwa asilimia 25, kutoka asilimia 71 mwaka 2014 hadi asilimia 46 mwaka 2017.

“Kipengele cha pili kilihoji kama wananchi wana haki na uhuru wa kueleza maoni yao,  nchini Tanzania,  idadi ya watu waliokiri kuwa huru ilishuka kutoka asilimia 71 mwaka 2014, hadi kufikia asilimia 46  mwaka 2017,” inaonesha ripoti hiyo.

Nchini Kenya, idadi hiyo imepungua kwa asilimia 10, kutoka asilimia 55 mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 45 mwaka 2017, wakati nchini Uganda, idadi hiyo ilipungua kwa asilimia 26, kutoka asilimia 66 mwaka 2014 hadi asilimia 40 mwaka 2017.

Wakati huo huo, ripoti hiyo imeonesha kuwa, asilimia kubwa ya watu waliohojiwa nchini Tanzania, kama serikali ina haki ya kudhibiti vyombo vya habari, waliafiki.

Na kuwa, asilimia 58 ya waliohojiwa walipendekeza serikali idhibiti mienendo ya vyombo vya habari. Kwa upande wa Kenya asilimia 14 waliafiki na Uganda asilimia 18.

Pia, asilimia 42 ya waliohojiwa Tanzania walipendekeza vyombo vya habari viachwe huru, Kenya ikiwa na asilimia 85 na Uganda asilimia 81.

Aidha, Ripoti hiyo ya Twaweza imeonesha kwamba, watu 6 kati ya 10 wanaimani na habari zinazochapishwa katika vyombo vya habari.

Ripoti hiyo imejikita katika vipengele vitatu, cha kwanza kilihoji kama serikali ina haki ya kuzuia vyombo vya habari, kuchapisha habari zinazodhaniwa kwamba ni hatari kwa jamii.

Au, vyombo vya habari vina haki ya kuchapisha mawazo au maoni, pasipo kuzuiwa na serikali.

Na cha pili kilihoji, kama wananchi wana uhuru wa kueleza maoni yao. Wakati cha mwisho, kilihoji kama vyombo vya habari vinatumia uhuru wao kuchapisha habari za ukweli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaanika madudu miradi ya ujenzi, moundombinu

Spread the loveCHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi juu ya uelekeo wa...

Habari za Siasa

Samia ashuhudia utiaji saini ujenzi wa minara 758 ya bilioni 265

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa kampuni za...

error: Content is protected !!