August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yapaa kuelekea Misri, watano waachwa

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba imeondoka nchini hii leo tarehe 14 Julai 2022 kuelekea nchini Misri kwa ajili ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa mshindano, huku baadhi ya wachezaji wakisalia jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kambi hiyo ya Simba itakwenda kudumu kwa wiki tatu, katika jiji la Ismailia ambapo itambatana na baadhoi ya michezo ya kirafiki.

Akieleza sababu ya kuanza maandalizi mapema Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally alisema kuwa kikosi chao kina idadi kubwa ya wachezaji wapya sambamba na benchi jipya la ufundi hivyo wanataka wazoeane kabla kuanza kwa mashindano.

“Tumeanza mandalizi mapema kwa sababu tuna sehemu kubwa ya wachezaji wapya, kocha mpya na benchi la ufundi jipya ni bora tuanze maandalizi mapema ili kutengeneza muunganiko.” Alisema msemaji huyo

Kwenye safari hiyo Simba iliacha wachezaji watano jijini Dar es Salaam, ambao wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), kitakachoingia kambini siku ya kesho tarehe 15 Julai mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Wachezaji hao walioachwa ni Aishi Manula, Mohamed Hussein, Mzamilu Yassin, Kennedy Juma na Kibu Denis.

Kwa mujibu wa Ahmed alisema kuwa, wachezaji hao watajiunga na wenzao mara baada ya kumaliza majukumu yao ya timu ya Taifa.

Taifa Stars itashuka dimbani kwenye mchezo wa kwanza tarehe 23 Julai, kwenye mchezo dhidi ya Somalia na marudiano itakuiwa tarehe 30 Julai 2022.

Michezo yote hiyo miwili itapigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!