Monday , 8 July 2024
Home Kitengo Biashara Shilole balozi mpya Oryx gesi kuhamasisha matumizi nishati safi
BiasharaHabari Mchanganyiko

Shilole balozi mpya Oryx gesi kuhamasisha matumizi nishati safi

Spread the love

KAMPUNI ya Gesi ya Oryx imemtangaza Mama Lishe, Zuwena Mohamed maarufu Shilole (Shishifood) kuwa balozi wao katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kupikia kupitia mitungi ya gesi nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Lengo la Oryx kumpa Ubalozi Shilole unalenga kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu ambaye ameweka malengo kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania iwe inatuminia nishati safi ya kupikia.

Mama Lishe na Msanii Zuwena Mohammed maarufu Shilole (katikati) akisisitiza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya Kampuni ya Oryx Gas Tanzania kumtangaza kuwa Balozi wao .Kulia ni Meneja Mauzo na Masoko wa Oryx Gas Shaban Fundi na Kulia ni Meneja Miradi ya Nishati safi Oryx Gas Peter Ndomba.

Akizungumza leo Alhamisi kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Meneja Mauzo na Masoko wa Oryx Gas, Shaban Fundi amesema wameamua kumchagua Shilole kwa sababu ni miongoni mwa wadau wanaohamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Amesema kupitia kwa Shilole wanaamini kuna wengine ambao walikuwa nyuma kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia kuendelea kutumia gesi za Oryx kupikia.

“Tunafamu Shilole amekuwa mjasiriamali maarufu, anamiliki migahawa ya Shishifood katika miji ya Dar es Salaam na Dodoma, amekuwa mama Lishe wa kisasa na muumini  mzuri wa kutunza mazingira.

“Oryx tunaona fahari kumtangaza Shilole kuwa balozi wetu katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ili kwa pamoja kufikia malengo ya Rais Samia ya kuhamasisha nishati safi ya kupikia nchini,” amesema.

Kwa upande wake Shilole ambaye pia ni Msanii maarufu nchini, amesema yupo tayari kushirikiana na wadau wengine kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Amesema Kampuni ya Oryx imekuwa ikiweka jitihada kubwa kuhamasisha matumizi nihati safi ya kupikia kwa Mama lishe na baba lishe nchini, hivyo ameona kuna umuhimu mkubwa wa kutoa ushirikiano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mwabukusi awaomba wanasheria kususia uchaguzi TLS

Spread the loveWakili Boniface Mwabukusi amesema kitendo cha kuenguliwa kugombea Urais wa...

Biashara

Unaijua namba 7 ya maajabu? Inatumika hivi kwenye kasino

Spread the love Unataka kuwa Milionea na hujui pa kuanzia? Nisikilize mimileo...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yajidhatiti kuendelea kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tz, Comoro

Spread the loveBenki ya NMB imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuimarisha uhusiano...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ufaransa wapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi

Spread the loveWapiga kura nchini Ufaransa leo Jumapili wanapiga kura katika duru...

error: Content is protected !!