Sunday , 30 June 2024
Home Kitengo Biashara Serikali yasitisha ukaguzi mashine EFD, kero 41 zaibuliwa
BiasharaHabari za SiasaTangulizi

Serikali yasitisha ukaguzi mashine EFD, kero 41 zaibuliwa

Mashine EFD
Spread the love

Serikali imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za kielekroniki (EFD) na ritani za kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia Mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Dar es salaam wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumatatu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya Wafanyabiashara.

Kikao hicho kiliitishwa na Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba na kuhudhiriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

“Wafanyabiashara walionesha changamoto ya ukosefu wa nyaraka hususani bandarini ambayo inasababisha makadirio ya kodi ambayo sio sahihi lakini pili ukokotoaji wa kiwango cha kodi wanacholipa, tatu ni uwepo wa Machinga katika maduka wanayouza na nne suala la kamatakamata inayoendeshwa na TRA na nne walionesha changamoto ya muswada wa sheria ya fedha.

“Bado ya majadiliano ya kina tunakubaliana kuanzia tarehe 1 Julai 2024 TRA itakuwa na mfumo mpya wa nyaraka ambao utatumika vizuri katika kuhakisha Wafanyabiashara wanapata makadirio sahihi kwa maana ya mfumo wa stakabadhi na marisiti yake,” amesema

Pili amesema TRA inasitisha oparesheni zake maarufu kama kamatakamata mpaka itakapokamilisha utaratibu huu ili kuweka utaratibu mzuri wa kukusanya mapato hususani katika suala la nyaraka, kuhusu ukokotoaji wa kodi ni suala la kisheria na sisi kaam Serikali tumelichukua ili kuboresha zaidi mfumo  wa ukokotoaji wa kodi hususani bandarini.

Kuhusu wamachinga, amesema Serikali inaendelea kuwapanga ili wakae maeneo sahihi ambayo hayaingilii watu wenye maduka ili kila mtu afanye biashara na alipe kodi ya serikali.

“Tano tumewataarifa wenzetu kuwa muswada washeria wa fedha wa mwaka 2024 haujapitishwa, kinachoendelea sasa ni kwamba kamati ya bunge ya bajeti imeita wadau wapokee maoni na niwahakikishie wabunge watazingatia maoni yao kabla sheria haijapitishwa,” amesema.

Amesema amesema Kamati iliyoundwa na Waziri mkuu, Kassim Majaliwa iliibua changamoto 41 ambazo zinawakabili wafanyabishara.

“Changamoto 35 ni mambo ya utendaji, sita ni mambo ya sheria na sera mbalimbali ambazo zote zinaendelea kufanyiwa kazi. Kwa mfano moja walitaka tuanze kutambua biadhaa nane kama mfano wa kukokotoa kodi. Serikali inafanyia kazi changamoto zote zilizoibuliwa kamati ya waziri mkuu,” amesema.

Amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya kufanya biashara nchini kwani nafasi ya Soko la Kariakoo katika Tanzania ni muhimu sana hivyo TRA wameelekezwa waendelee kuilinda hadhi ya Kariakoo kama kitovu muhimu cha biashara Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Meridianbet waadhimisha siku ya Wajane Duniani kwa kutoa misaada mbalimbali

Spread the love Siku ya leo Meridianbet wameamua kuadhimisha siku ya wajane...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lema: Nimesikitishwa na uamuzi wa Msigwa

Spread the loveMJUMBE wa Kamati Kuu Chadema, Godbless Lema ameeleza kushtushwa na...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Kura mbili zamhamishia Mch. Msigwa CCM

Spread the loveAliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini na mjumbe wa zamani wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Tanzania yaiuzia Zambia mahindi tani 650,000

Spread the loveTanzania imeuza mahindi tani 650,000 nchini Zambia ikiwa ni utekelezaji...

error: Content is protected !!