Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko  SBL yakabidhiwa tuzo na Waziri Mkuu kwa uwekezaji kwenye miradi ya maji safi
Habari Mchanganyiko

 SBL yakabidhiwa tuzo na Waziri Mkuu kwa uwekezaji kwenye miradi ya maji safi

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameikabidhi Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), tuzo ya kutambuliwa mchango wao kwenye sekta ya maji kutoka kwa serikali na Water Aid Tanzania hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Waziri Mkuu Majaliwa amekabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ambayo kwa upande wa kampuni ya SBL, ilipokelewa na Meneja wa Mawasiliano na Mambo Endelevu wa SBL, Rispa Hatibu.

SBL imepokea tuzo hiyo kutokana na ufadhili wake wa miradi ya maji kwa lengo la kuleta afueni katika maeneo yanayokabiliwa na uhaba wa maji nchini, imekuwa moja ya malengo muhimu ya kampuni hiyo kama sehemu ya juhudi za uwajibikaji wake kijamii kwa miaka 13 sasa.

Hadi sasa, SBL imefadhili utekelezaji wa jumla ya miradi 24 ya maji katika sehemu mbalimbali za nchi, jambo ambalo kimsingi limehakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa zaidi ya watanzania 2,000,000.

Dhamira ya SBL katika kufadhili miradi ya maji inalingana na nguzo yake ijulikanayo kama ‘Maji ya Uhai’ ya kampuni hiyo ambapo lengo la kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yanayokabiliwa na uhaba wa maji. Kwa kutambua umuhimu wa kushirikiana na wadau kimkakati katika utekelezaji wa miradi, SBL imekuwa ikishirikiana na Water Aid Tanzania, shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na utoaji wa maji safi na uhamasishaji wa usafi.

Shughuli ya kukabidhi tuzo hiyo ilifanyika wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Programu ya Nchi ya Water Aid Tanzania, tukio lililokusanya wadau wa maji kutoka sekta binafsi na sekta ya umma. Kauli mbiu ya uzinduzi wa mkakati wa programu ya nchi ilikuwa ‘Kumaliza Mgogoro wa Maji, na Usafi kwa Pamoja – kwa kila mtu, kila mahali.’ Tukio hilo lilijumuisha majadiliano ambayo yalilenga kwenye mada ya ziada, ‘Kuchunguza kwa kina mazoezi yetu ya utoaji; Hatua ya kubadili kudai mahitaji ya WASH ya kibaolojia na ya vitendo kwa wanawake na wasichana.

Akizungumza kuhusu kupokea tuzo hiyo, Meneja wa Mawasiliano na Mambo Uendelevu wa SBL, Rispa Hatibu alisema, “Tumekuwa tukiongoza kufadhili miradi kadhaa ya maji katika maeneo yanayokabiliwa na uhaba wa maji kwa kushirikiana na sekta binafsi kama Water Aid pamoja na taasisi za serikali, na malengo makuu yakiwa ni kutoa maji safi na salama kwa Watanzania.

“Tumewafikia zaidi ya watu milioni 2 kupitia miradi yetu, lengo letu ni kuendelea kufikia idadi kubwa ya walengwa nchi nzima. Hii ni sehemu ya nguzo yetu ya ‘Maji ya Uhai’ ambayo tumekuwa tukiitekeleza kwa miaka 13 sasa katika sehemu mbalimbali nchini. Kitendo cha SBL kupokea tuzo kutoka kwa serikali na wadau kutoka sekta ya maji kunathibitisha jinsi miradi yetu ya maji ilivyokuwa na matokeo chanya makubwa kwa jamii ya Watanzania.”

Hatibu aliongeza kuwa, mbali na miradi ya maji iliyokamilika, kampuni hiyo ya bia imekamilisha mradi mwingine wa maji wenye thamani ya milioni 380 katika wilaya ya Handeni, mkoani Tanga. “Hii itakuwa ni hatua nyingine kubwa sio tu kwa SBL bali pia kwa jamii ya Handeni ambayo sasa itapata maji safi na salama, na kuongezea hilo, tumewapa pia ujuzi wa maswala ya WASH ambao utawawezesha wakazi hao kulisimamia kiendelevu bwawa hilo la maji.”

Kwa upande wake, Meneja wa Water Aid Tanzania, Anna Mzinga alisema SBL imekuwa mstari wa mbele katika kufadhili miradi ya maji katika maeneo yanayokabiliwa na uhaba wa maji nchini, ikifanya uwekezaji wa mamia ya mamilioni katika miradi hiyo. “SBL imekuwa moja wa wadau muhimu kwenye utekelezaji wa miradi ya maji, dhamira yao na jitihada ni za hali ya juu, na ndiyo maana tumewashukuru kwa msaada wao usiokoma katika kuimarisha juhudi za serikali katika kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwenye jamii zetu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!