Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Samia amteua Diallo mwenyekiti bodi TFRA
Habari Mchanganyiko

Samia amteua Diallo mwenyekiti bodi TFRA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Dk. Anthony Diallo
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mwanza, Antony Diallo, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA).Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo tarehe 14 Februari 2023, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus.

Yunus kupitia taarifa hiyo amesema kuwa, Diallo anachukua nafasi ya Profesa Antony Mshandete, ambaye amemaliza muda wake, ambapo uteuzi wake ulianza tarehe 9 Februari mwaka huu.

Mbali na uteuzi wa Diallo, Rais Samia amemteua Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali George Marwa Waitara, kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi Tanzania (TANAPA).

Kwa mujibu wa taarifa ya Yunus, uteuzi wa Jenerali Waitara, umeanza tarehe 13 Februari 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

error: Content is protected !!