Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia: Wizara afya fanyeni tathmini hali ya Uviko-19
Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia: Wizara afya fanyeni tathmini hali ya Uviko-19

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Afya kufanya tathmini ya hali ya ugonjwa wa Uviko-19 nchini na kutoa utaratibu kama watu waendelee kuvaa barakoa au lah!

Pia, amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuwa janga hilo bado lipo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 3 Septemba, 2022 wakati akihutubia kilele cha maadhimisho ya siku ya Kizimkazi yanayofanyika katika wilaya ya Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Maadhimisho hayo yalilandana na kauli mbiu isemayo, “Royal tour na uchumi wa buluu ni chachu ya maendeleo yetu, umoja wetu ni nguzo bora ya maendeleo yetu, tushikamane ili tupate maendeleo”.

Akihutubia wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo, amesema kutokana na hali aliyoiona kwenye uwanja huo ambapo wananchi hawajavaa barakoa inaonyesha kuchoshwa nazo.

“Nilipoingia eneo hili leo nilikuja na barakoa yangu, nikatazama uwanja sikuona hata moja amevaa barakoa isipokuwa mimi na timu yangu niliyokuja nayo, mimi nikaanza kutoa yangu, wanasema ukienda Roma fanya kama wanavyofanya, nikaanza kutoa yangu (barakoa), na wengine wakanifuata.

“Hii inaonesha tusijiachie sana, bado janga lipo, tumejifunza kuishi nalo lakini bado janga lipo.

“Niwaombe sasa wizara ya afya waangalie mwenendo tunaokwenda nao, kwa sababu kitendo cha watu wote hawa kuacha barakoa ina maana wamechoka nazo,” amesema.

Amesema kutokana na hali aliyoiona kwenye uwanja huo ambapo wananchi hawajavaa barakoa inaonyesha kuchoshwa nazo.

“Kuacha barakoa watu wote hawa inaonyesha watu wamechoka nazo, watu wamechoka nazo, niwaombe sasa Wizara ya Afya waangalie mwenendo huu tunaokwenda nao, lakini sasa watathmini hali ilivyo halafu watuambie tuendelee kuwa nazo au kwa muda tupumzike,” amesema Rais Samia ambaye alikuwa Kizimkazi eneo ambako ndiko alipozaliwa.

Hata hivyo, Rais huyo amewataka wale ambao hawajachanja wachanje kwa hiari ili kuweza kuwa kwenye hali nzuri ya kuzuia maambukizi ya janga hilo.

“Nataka niwaambie msijiachie sana, bado janga lipo, tumejifunza kuishi nalo lakini ninalotaka kuwaambia janga bado lipo chanjo bado ipo, kama hujachanja chanja ni bure hulipi hata shilingi nenda kachanje janga bado lipo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari Mchanganyiko

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

error: Content is protected !!