Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Dk. Mwinyi amwagia sifa Dk. Mwele “ni mtu wa karibu sana kwangu”
Habari Mchanganyiko

Rais Dk. Mwinyi amwagia sifa Dk. Mwele “ni mtu wa karibu sana kwangu”

Dk. HUssein Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Spread the love

 

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema marehemu Dk. Mwele Malecela alikuwa ni mtu wa karibu sana kwake binafsi na familia yake hivyo msiba huo umemgusa sana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Dk. Mwinyi ameongeza kuwa alimfahamu vizuri Dk. Mwele wakati wazazi wao, Mzee Samuel Malecela (waziri mkuu mstaafu) na Mzee Ali Hassan Mwinyi (rais mstaafu) wakifanya kazi pamoja.

“Sisi familia zetu zilikuwa karibu, tulikuwa marafiki, tulikuwa majirani, tulikuwa kama ndugu,” amesema.

Akizungumza katika ibada ya kuaga mwili wa Dk. Mwele iliyofanyika leo tarehe 19 Februari katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Dk. Mwinyi amesema amemfahamu vizuri Dk. Mwele katika shughuli zao za kazi.

Amesema wakati akiwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Mwele alikuwa akifanya kazi NIMR katika nafasi mbalimbali hadi kufikia kufikia nafasi ya Mkurugenzi Mkuu.

“Kwa kweli wote waliomzungumzia Dk. Malecela maisha yake ya kazi, wamesema yote, huyu ni mtu ambaye alikuwa ni mtu ambaye committed, dedicated na very professional

“Binafsi wakatin nikifanya naye kazi nimemuona alivyokuwa akijituma, akitaka mambo yawe na yafanikiwe na kwa kweli ameipa sifa nchi hii kwa kwa program alizozifanya akiwa NIMR.

“Kila mara nilipokuwa nikizingumza na washirika wetu wa maendeleo, taasisi za umoja wa mataifa, walikuwa wakimwagia sifa Dk. Mwele kwa kazi kubwa aliyokuwa akiifanya hususani katika progamu hgizi za matende pamoja na ile ya NTDs.

“Kwa kweli sina maneno zaidi ya kuongeza, zaidi ya kusema marehemu Dk. Mwele ameitumikia nchi yake, amefanya kazi miaka 30 akiitumikia nchi yake, kwa kweli sisi sote tunapaswa tujiulize endapo tunaweza kufikia yale ambayo Dk. Mwele ameyafikia,” amjesema.

Aidha, amesema mbali upande wa kazi, kama binadamu, Dk. Mwele alikuwa ni mtu mwenye utu ndio maana leo wamejumuika kila mmoja kuzungumzia alivyoguswa.

“Alikuwa karibu sana na watu, alikuwa anapenda kusaidia, siwezi kusema yote ila niseme tunaambiwa ibada sio kuyafanya tuliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na kuyaacha aliyotukataza, bali pia kuwatumikia watu, hilo Dk. Mwele alifanikiwa.

“Viongozi wa dini wanatuambia kwamba katika kifo kuna mawaidha, itoshe sisi tuliobaki kujiuliza siku ambayo wakati wetu utafika tutazungumzwa kama haya yanayozungumzwa kuhusui Dk. Mwele?

Dk. Mwele Malecela, Mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika vya Shirika la Afya Duniani (WHO)

“Lakini vilevile tunaambiwa kwamba maisha ni hadhithi, tujitahidi kuacha hadithi njema kama hii tunayozungumza hapa kuhusu mwenzetu,” amesema.

Amesema katika kipindi hiki, kupata maneno mazuri inakuwa ngumu lakini Watanzania wana wajibu mmoja wa kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

“Vilevile tuna wajibu wa kukuombeeni ninyi faimilia Mwenyezi Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki ncha majonzi.

“Msiba huu umetugusa sote, kwa sababu huyu aliyetangulia mbele ya haki ni mtu wa karibu sana kwangu mimi binafsi na kwa familia yangu,” amesema Rais Dk. Mwinyi.

Dk. Mwele (58) ambaye hadi umauti unamfika tarehe 10 Februari, 2022 alikuwa Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele katika Shirika la Afya Duniani (WHO).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!