Sunday , 30 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi Moshi wamng’ang’ania Malisa, wafufua madai ya Waziri Mkenda
Habari za SiasaTangulizi

Polisi Moshi wamng’ang’ania Malisa, wafufua madai ya Waziri Mkenda

Godlisten Malisa
Spread the love

WAKILI wa Mwanaharakati Godlisten Malisa, Hekima Mwasipu amesema mteja wake anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kuwa Lucas Paul Tarimo aliyedaiwa kumuua mkewe, alikuwa mfanyakazi wa Mbunge wa Rombo, Prof. Adolf Mkenda ambaye pia ni Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI leo Ijumaa kwa njia ya simu, Mwasipu amesema Malisa alisafirishwa jana tarehe 6 Juni mwaka huu kutoka Dar es Salaam kuelekea Moshi baada ya kukamatwa nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokwenda kusikiliza kesi yake.

Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.

Katika kesi hiyi namba 11805 /2024 Malisa anashtakiwa pamoja na aliyekuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob ya kuchapisha taarifa za uzushi kwenye mtandao wa ‘X’  .

Akifafanua zaidi, Mwasipu amesema Malisa alisafirishwa jana Ijumaa mchana kutoka Dar es Salaam na kufika Moshi saa nne usiku kisha kuanza kuhojiwa saa saba kasoro usiku.

“Alihojiwa kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kuhusu bwana mmoja anayeitwa Paul Tarimo aliyesemekana kumuua mkewe anayeitwa Beatrice Minja huko Rombo.

Lucas Paul Tarimo

“Malisa alisema inasadikika huyu Tarimo alikuwa anafanya kazi kama ‘Shamba boy’ kwenye shamba la Profesa Adolf Mkenda hivyo anatuhumiwa kusambaza taarifa za uongo kwani polisi wanadai aliyemuua Beatrice hakuwa mfanyakazi wa Mkenda.

“Polisi hawana ubishi kuwa bwana Paul alimuua Beatrice na hawabishi kuwa Paul alijiua kwenye kituo cha polisi, hoja yao kwanini alisambaza taarifa za uongo kwamba bwana Paul alikuwa mfanyakazi wa Profesa Mkenda” amesema Wakili Mwasipu.

Hata hivyo, Profesa Mkenda aliwahi kukanusha kupitia mkutano wake na waandishi wa habari kuwa Tarimo hakuwa mfanyakazi wake.

Mwasipu amesema kuwa mpaka sasa Jeshi hilo halijampa dhamana Malisa na kwamba zipo taarifa nyingine kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka (DCI), yupo njiani akitokea Dodoma kwa ajili ya kumhoji

Amesema kuwa yeye na Wakili Peter Kidumbuyo tayari wanatayarisha kesi kwa ajili ya kulishinikiza jeshi la Polisi kuamuachia Malisa.

“Tumeanza kuandika shauri la kuiomba mahakama kulilazimisha Jeshi la Polisi kumuachia kwa sababu wanamshikilia kinyume cha sheria ilihali tuhuma zake zinadhaminika.

Beatrice Minja.

Mtuhumiwa wa mauaji ya Beatrice Minja, Lucas Paul Tarimo aliyefariki tarehe 2 Januari mwaka huu kutokana na madhara yaliyodaiwa kuwa sumu ya kuulia wadudu aliyokunywa, alikamatwa  tarehe 31 Disemba mwaka jana kwa tuhuma za kumuua mkewe Beatrice Minja.

Polisi walimkamata Tarimo katika kijiji cha Jema, wilaya ya Ngorongoro akijaribu kutorokea Kenya. Polisi walidai alikua na dawa ya kuulia wadudu na alipowaona alikunywa kidogo lakini wakamuwahi na kumkimbiza hospitali

MwanaHALISI limezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Simon Maigwa ambaye amesema bado hajafuatilia suala hilo kwa kuwa yupo kwenye msafara wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, mkoani humo, Dk. Emanuel Nchimbi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Tanzania yakubali kukutana na mabalozi 9 kutatua changamoto za kikodi

Spread the loveSerikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na...

error: Content is protected !!