Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko PAC: Bila hati, eneo sio lako
Habari Mchanganyiko

PAC: Bila hati, eneo sio lako

Spread the love

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imemuagiza Katibu Mkuu wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi kuhakikisha wanafikia lengo la kutoa hati miliki za ardhi kwa wananchi ambao vipande vyao vya ardhi vimetambuliwa na kupangwa kulingana na matumizi ya ardhi mkoani Shinyanga. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Pia imemuagia kuhakikisha malengo ya Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) unaotekelelezwa na Wizara hiyo katika Manispaa ya Shinyanga yanatekelezwa kabla ya kufika mwezi Juni 2024.

Hasunga ametoa maagizo hayo leo wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) unaotekelelezwa na Wizara hiyo katika Manispaa ya Shinyanga ili kuangalia hatua zilizofikiwa pamoja na thamani ya fedha iliyotumika kutekeleza mradi huo katika manispaa hiyo.

Wajumbe wa kamati hiyo walitembelea utekelezaji wa mradi huo pia katika kata ya Ibadakuli na Kibada na kujionea wananchi wakihakiki taarifa zao ambazo zilichukuliwa wakati wa utambuzi na maeneo walipokuwa wanaweka alama za utambuzi wa maeneo (bicorns).

“Tumetembelea maeneo mbalimbali, tumeona wanavyotekeleza huu mradi tumepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi na ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Ibadakuli iliyopo Manispaa ya Shinyanga, Hasunga amesema kumalizika kwa migogoro ya ardhi kupitia mradi huo wa wananchi wa manispaa ya Shinyanga kutatoa fursa wananchi kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao ikiwemo kujenga nyumba katika maeneo wanayomiliki kwa kuwa na hati miliki za ardhi.

“Ukiwa na hati ya kumiliki eneo hapo hakuna mtu atakayekuondoa tena, hapo ndipo utakapoona manufaa ya kumiliki ardhi, hiyo hati itakusaidia mambo mengi. Unaweza kwenda benki kupata mikopo kufanya shughuli zako za maendeleo, utajenga nyumba na kufanya shughuli nyingine za maendeleo ukiwa na hati yako. Bila hati, eneo sio lako”

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga amewashukuru wajumbe wa Kamati hiyo kwa ushirikiano wanaoendelea kupata katika kutekeleza majukumu yao na wamepokea maelekezo na ushauri wa kamati na kuahidi kuyafanyia kazi kama walivyoelekeza.

Aidha, Sanga amesema utekelezaji wa Mradi wa LTIP umefikia asilimia 51 nna kazi hiyo itakamilika katika halmashauri ya Shinyanga kama ilivyoelekezwa na Kamati hiyo.

Akifafanua kwa Kamati hiyo Mratibu wa Mradi wa LTIP, Joseph Shewiyo amesema kwa Manispaa ya Shinyanga mradi huo hadi kukamilika kwake utagharimu kiasi cha Sh bilioni 1.4  ambapo Sh bilioni 1.3 imepangwa kwenye shughuli za urasimishaji na Sh milioni 21.4 zimepangwa kujenga alama za msingi za upimaji.

Amesema hadi sasa Sh milioni 452 zimetumika kwenye kazi ya utambuzi, upangaji na upimaji, kununua vifaa, ujenzi wa alama za msingi 10 na elimu kwa umma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

error: Content is protected !!