Thursday , 4 July 2024
Home Kitengo Biashara NSSF yawataka wastaafu watarajiwa kuhakiki taarifa zao
BiasharaHabari Mchanganyiko

NSSF yawataka wastaafu watarajiwa kuhakiki taarifa zao

Spread the love

Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) umewataka watumishi wanaotarajiwa kustaafu kuanza kujiandaa ikiwa ni pamoja na kuhakiki taarifa zao za msingi sambamba na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha hali itakayosaidia kupunguza changamoto za maisha pindi wanapostaafu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa mafao wa NSSF Ilala, Mrisho Mwisimba wakati akimuwakilisha mkurugenzi wa uendeshaji katika warsha iliyolenga kutoa elimu kwa watumishi wanaotarajia kustaafu kutoka katika mkoa wa Temeke ambapo pia amewasisitiza kuanzisha miradi salama ya uwekezaji ili kuwa na uhakika wa kipato endelevu.

Kwa upande wake Meneja idara ya biashara wa Benki ya Biiashara ya taifa (TCB), Emmanuel Nyange ambao pia walihudhuria mafunzo hayo kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha katika mafao, amesema TCB imeamua kusimama na wastaafu kwa miaka 10 sasa ikijikita katika kutatua changamoto wanazokutana nazo wastaafu kwa kuanzisha akaunti maalumu ya Kivulini isiyo na makato yeyote wala gharama za uendeshaji, lengo likiwa ni kumnusuru mstaafu.

Nyange ameongeza kuwa sambamba na hayo TCB imeanzisha huduma za pesheni advance inayomuwezesha mstaafu kupata fedha ya kujikimu kwa kutoa suluhu kwa tatizo analokutuna nalo,ila pia kuna huduma ya mkopo usio na masharti yeyote.

Aidha, kwa wastaafu watarajiwa TCB wanatoa huduma za fixed akaunti huku asilimia yake ikiwa ni mpaka asilimia 11 kwa mwaka, kupitia akaunti ya kivulini bado wastaafu wakipata majanga au ulemavu wa kudumu wanapewa fidia,na sababu kuu ni adhimio la serikali kuweza kufikia makundi yote katika huduma za ujumuishaji wa kifedha.

Huduma hizo zote zinatolewa katika mkitadha wa kutatua changamoto wanazopitia wastaafu hivyo kuwasihi wastaafu watarajiwa kuhakikisha wanasamehe na kuachana na yaliyopita na zaidi wafungue akaunti na tcb ili waweze kupata huduma zote hizo.

Kwa upande wake Afisa Mafao mkuu wa NSSF, Shakira Masoli amewasisitiza watumishi kujiandaa kustaafu kwa kuhakikisha wanapeleka na wanahakiki taarifa zote za msingi ili kuepusha usumbufu pindi wanapostaafu.

Naye mmoja wa wanufaika wa NSSF, Damas Nungu ameutaka mfuko huo kupunguza kikokotoo cha awali anachopewa mstaafu huku akiwahimiza waajiri kupeleka michango ya watumishi wao kwa wakati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko awataka Watanzania kulinda viumbe hai baharini

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia, Nyusi wapongeza mkakati wa utanuzi PBZ, yakaribishwa kufungua tawi Msumbiji

Spread the loveRais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepongeza jitihada zinazofanywa na...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Bwire Mtendaji mpya DAWASA

Spread the loveMhandisi Mkama Bwire ameteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Afisa Mtendaji...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia aahidi ushirikiano Rais mpya TEC

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza...

error: Content is protected !!