Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yapongeza ushirikiano wa Jeshi la Polisi
Habari Mchanganyiko

NMB yapongeza ushirikiano wa Jeshi la Polisi

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kusimamia usalama na ulinzi wa taifa jukumu ambalo Benki ya NMB imesema limechangia kwa kiasi kikubwa kuifanya taasisi hiyo kuwa kinara wa huduma za kifedha nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Pongezi hizo zilitolewa jana Jumanne, tarehe 30 Agosti 2022, Moshi mkoani Kilimanjaro na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa maafisa waandamizi wa jeshi hilo ambako alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali wa maendeleo zikiwemo taasisi za fedha.

“Tunalipongeza jeshi letu la polisi kwa kuendelea kusimamia usalama na amani nchini ambayo ni msingi mkubwa wa maendeleo wa mataifa yote duniani,” alisema Rais Samia alisema kwenye hotuba yake ya kukifungua kikao kazi hicho kwenye Chuo Cha Polisi.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Rashid Masauni, alisema mchango wa NMB kulisaidia Jeshi la Polisi kuwahudumia watanzania ni wa kuigwa akitolea mfano wa benki hiyo kukubali kugharamia ununuzi wa samani za kituo chake kipya kitakachozinduliwa hivi karibuni huko Zanzibar.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, aliuambia mkutano huo kuwa kutokana na Jeshi la Polisi kuwa chombo nyeti kinachosimamia ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao, benki hiyo itadumisha ushirikiano nalo na kulipa kipaumbele ili utendaji kazi wake uwendelee kuwa wa ufanisi na tija kwa taifa.

Moja ya maeneo muhimu kulifanikisha hilo, alifafanua, ni kulisaidia kukusanya mapato.

“Ushiriki wa NMB katika ukusanyaji mapato ya Serikali ni mkubwa sana. Makusanyo zaidi ya TZS Trilioni 9.6 yalifanyika kati ya mwaka 2018 na 2021 ikiwa mwaka jana pekee tulikusanya TZS trilioni 3.7. Na kwa Jeshi la Polisi makusanyo kwa mwaka 2021 yalikuwa zaidi ya TZS bilioni 40,” alisema Zaipuna alibainisha kwenye wasilisho lake.

Aliwaambia washiriki wa mkutano kuwa jeshi hilo lina mchango mkubwa katika mafanikio yao kama benki kiongozi wa huduma za kifedha nchini kwa kuiunga mkono kibiashara.

Huku akilipongeza jeshi la polisi kwa kuyalinda matawi yote 227 ya NMB yaliyo nchi nzima, alisema suluhisho walizonazo kwa ajili ya jeshi hilo ni pamoja na mikopo ya mishahara na nyumba, na huduma za bima na uwekezaji.

Akihitimisha wasilisho hilo, Zaipuna aliliomba Jeshi la Polisi kuendelea kushirikiana na benki hiyo kama mshirika mkubwa wa kifedha na kusaidia serikali kufanikisha ajenda ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.

Pia, alibainisha kuwa NMB ina uzoefu na utaalamu wa kutosha kuweza kukidhi mahitaji ya chombo hicho kwenye upande wa suluhisho za kidijitali ambazo Rais Samia alisema ni muhimu kwenye mageuzi ya kuliboresha jeshi hilo.

“NMB inaongoza sokoni katika matumizi ya teknolojia kuwahudumia wateja ambapo zaidi ya asilimia 95 ya miamala yake inafanyika kidijitali nje ya matawi kupitia mawakala zaidi ya 10,000, ATMs zaidi ya 800 na huduma nyingine mbadala za kibenki kama NMB Mkononi na Internet Banking,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Total Energies yawekeza bilioni 17 kusambaza gesi ya kupikia

Spread the loveILI kurahisisha upatikanaji wa gesi ya kupikia kwa gharama nafuu...

error: Content is protected !!