Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mvua yasababisha maafa Morogoro
Habari MchanganyikoTangulizi

Mvua yasababisha maafa Morogoro

Spread the love

MVUA mkubwa iliyoanza kunyesha usiku wa kuamkia leo Ijumaa, tarehe 13 Januari 2023 mkoani Morogoro, imesababisha maafa kwa wananchi wa baadhi ya maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko.Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Mafuriko ya mvua hiyo yamesababisha baadhi ya nyumba kubomoka, mali kusombwa na maji pamoja na kuingia katika makazi ya watu, hususan kwenye maeneo ya Kihonda, Soko la Chief Kingaru na Majengo Mapya.

Mbali na aza hizo, mvua hiyo imetajwa kusababisha foleni katika Barabara ya Morogoro-Dodoma, kutokana na maji kujaa barabarani.

 

Mkazi wa maeneo ya Majengo Mapya aliyejitambulisha kwa jina la Mkude, amewaeleza waandishi wa habari kuwa, baadhi ya vyombo vyake vya ndani vimesombwa na maji ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua hiyo.

“Kwa kweli hali ni mbaya sana, mvua imeleta athari kubwa imeanza kunyesha kuanzia saa usiku. Hatujalala kwa amani nyumba zote zimejaa matope ndani tunafanya kazi ya kuyatoa nje, vyombo vyote vimeondoka na maji na kama mnavyoona bado inaendelea kunyesha,” amesema Mkude.

Aidha, Serikali ya Mkoa wa Morogoro, imefika katika maeneo yaliyoathirika zaidi ya mvua hiyo kwa ajili ya kutoa msaada.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!