Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Biashara Mikopo ya bajaji Mbeya gumzo kwa vijana, washindana kujiimarisha kiuchumi
BiasharaUjasiriamali

Mikopo ya bajaji Mbeya gumzo kwa vijana, washindana kujiimarisha kiuchumi

Spread the love

VIONGOZI na wanachama wa kikundi cha Vijana Waendesha Bajaji (Viwaba) eneo la Mbalizi, katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya mkoani hapa wameeleza namna mkopo wa zaidi ya Sh60 milioni walioupata kutoka halmashauri ulivyowawezesha kujiajiri sambamba kujikwamua kimaisha.

Mkopo huo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali lililowataka wakurugenzi wa manispaa, majiji na halmashauri mbalimbali nchini kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Akieleza mafanikio na uwepo wa mikopo hiyo ya halmashauri, Katibu wa Viwaba, Anangisye Jengela amesema Viwaba ilianza na mtaji wa Sh milioni moja walipanda hadi kupatiwa Sh milioni sita lakini malengo yao hayakutimia.

“Mwaka jana tulikopeshwa Sh milioni 60.7 i na halmashauri kupitia mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na halmashauri. Baada ya kupata mkopo ule tuliutumia kununua bajaji kwa sababu wengi wa vijana wa hapa walikuwa wameajiriwa kuendesha bajaji za watu, binafsi,” amesema Jengela.

Jengela amesema kupitia mkopo huo, vijana wa Viwaba wamejiajiri na kujiendesha kimaisha bila kutegemea ajira kutoka kwa watu binafsi au Serikalini.

Amesema mbali na hilo, Viwaba imejikita kwenye kilimo cha alizeti baada ya kununua shamba la ekari moja.

“Mipango yetu ya baadaye kuanzisha kiwanda cha kuzalisha alizeti ambacho kikikamilika kitatoa fursa ya ajira kwa vijana wengi zaidi. Tumeshaanza kulima alizeti, lakini tukifanikiwa kupata eneo tutafanya kilimo kikubwa kitakachoajiri vijana wengi,” amesema Jengela.

Naye mjumbe wa Viwaba, Medson Mbilinyi amesema hadi sasa wamekwenda vizuri na mkopo wa halmashauri ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kubadilisha mwenendo wa maisha yao, tofauti na miaka iliyopita.

“Tunaipongeza Serikali kwa kutuona sisi vijana na kutupatia mikopo hii iliyotunufaisha kwa sababu tulianza shughuli zetu za bajaji tukiwa waajiriwa lakini sasa tumejiajiri wenyewe. Tunamshukuru sana Mama Samia Suluhu Hassan (Rais wa Tanzania) kwa kutuwezesha vijana Mungu ambariki,” amesema Mbilinyi.

Mbilinyi ameongeza kuwa “awali akifanya kazi kwa mtu binafsi kila siku ilinilazimu kupeleka Sh20,000 huku mwenyewe nikirudi nyumbani na Sh 5,000. Lakini tangu tumepata mkopo naweza kuingiza kati ya 35,000 au 40,000. Nikitoa fedha za mafuta nabaki na Sh 10,000 au 15,000 ya nyumbani na fedha ya rejesho napata.”

Mbilinyi amemshukuru kwa mara nyingine Rais Samia, akimueleza kuwa fedha ya mkopo ya asilimia 10 kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kwa halmashauri ya wilaya ya Mbeya imefika na watu wananufaika kupitia miradi mbalimbali.

Naye Jason Cheyo amesema kupitia mkopo wa halmashauri umemnufaisha kwa kupata bajaji mpya inayomuingizia fedha anazozitumia kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kusomesha mwanaye katika shule ya kisasa ya awali.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Orb of Destiny kutoka Meridianbet kasino ushindi kwa njia 14  

Spread the love  ORB of Destiny ni mchezo wa sloti kutoka kwa...

Biashara

Jiandalie Strawberry Cocktail yako nyumbani huku unacheza kasino 

Spread the love  UTAANDAA matunda yako unayotaka kutumia unaweza kutumia Strawberry, Cantaloupe...

Biashara

420 Blaze It chimbo jipya la kuchota mihela Meridianbet kasino 

Spread the love  JE, umewahi kucheza mchezo wa droo wenye droo 10?...

Biashara

Exim yawainua kiuchumi wanawake wajasiriamali kupitia mpango wa WEP

Spread the love  BENKI ya Exim kupitia Mpango wake wa Kuwawezesha Kiuchumi...

error: Content is protected !!