Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe achukua fomu urais, asema atamwaga cheche
Habari za Siasa

Membe achukua fomu urais, asema atamwaga cheche

Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya
Spread the love

WAZIRI wa zamani wa mambo ya nje, Bernard Membe amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama cha ACT-Wazalendo kimpitishe ili awanie urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)

Membe amechukua fomu hizo leo Ijumaa mchana tarehe 17 Julai 2020 katika Ofisi za ACT-Wazalendo zilizopo Magomeni jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu.

Shaibu amesema, Membe alifanya mazungumzo na ofisi ya katibu mkuu akieleza adhima yake ya kwenda kugombea urais wa Tanzania na mchakato wa ndani bado unaendelea.

Amesema mchakato huo umeanza tarehe 1 Julai 2020 na bado unaendelea.

“Wajibu wangu kama katibu mkuu ni kumkabidhi fomu,” amesema Shaibu

Soma zaidi hapa

Maalim Seif: Membe unaogopwa, gombea urais Tanzania

Baada ya kukabidhiwa fomu, Membe aliyewahi kuwa mbunge wa Mtama Mkoa wa Lindi akiwa na nyuso ya furaha wakati wote amesema, “napenda kutoa shukurani kwa ukaribisho mzuri alioupata ofisini kwake na kubwa lililonileta ni kuja kuitikia ombi la wanachama wa ACT-Wazalendo na Maalim Seif Sharif Hamad la kugombea urais.

“NImekabidhi ombi hilo kwa maandishi na nimekabidhiwa fomu ambazo nitakwenda kuzisoma na nitatekeleza vizuri sana, nitajaza vizuri sana, kwenye herufi kubwa nitaweka herufi kubwa,” amesema

Soma Zaidi hapa

Msajili aikamia ACT-Wazalendo, atishia kuifuta

Membe amesema, mpaka anachukua alikuwa peke yake na kutoa wito kwa wengine kwenda kuchukua fomu zipo nyingi “si kama wale wengine”

Amesema leo hana la kuongea zaidi, “siku nikirejesha fomu hizi nitakuwa na la kusema, nitamwaga cheche moja mbili tatu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!