Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Meli kubwa yenye magari 4,041 yawasili Dar
Habari Mchanganyiko

Meli kubwa yenye magari 4,041 yawasili Dar

Spread the love

 

BANDARI ya Dar es Salaam nchini Tanzania,l imeweka rekodi nyingine kwa kupokea meli kubwa kuwahi kufika bandarini hapo ikiwa na shehena ya magari 4,041. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Meli hiyo MV Frontier Ace yenye ukubwa wa GRT 52,276 na urefu wa mita 198.45 imewasili leo Ijumaa tarehe 8 Aprili 2022 ikitokea moja kwa moja nchini Japan.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewaongoza wafanyakazi na wafanyabiashara kuipokea meli hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi amesema, kati ya magari hayo 2,936 yanakwenda nje ya nchi na 1,105 yanabaki nchini.

“Hii ni meli kubwa kuliko meli zote iliyowahi kutia namba katika bandari ya Dar es Salaam,” amesema Hamissi na kusema meli kubwa iliyokuwa inashikilia rekodi ilitua Agosti 2021 ikiwa na magari zaidi 35,000.

Ametaja nchi yanakokwenda hayo 2,936 ni, Burundi, DR Congo, Malawi, Msumbiji, Sudan ya Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

“Bandari yetu imepata uaminifu na kuaminiwa kwa kutumiwa na nchi mbalimbali. Hii ni meli kubwa lakini kati ya 5 na 6 Aprili 2022 tumepokea meli zenye magari 4,343 ukijumlisha na hii ni 8,384 ndani ya siku tatu ni kubwa sana na tutaendelea kusonga mbele,” amesema Hamissi

“Huu ni mwanzo mzuri kwa TPA, kwani kwa maboresho yaliyofanyika na yanaendelea kufanyika tunatarajia kuhudumia shehena kubwa zaidi ya mizigo mchanganyiko, kichele na mafuta,” amesema Hamissi

Amesema shehena ya magari iliyohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Machi 2021 hadi Februari 2022 ilifikia magari 185,524 ambayo ni ongezeko la asilimia 2.2 ukilinganisha na lengo la kuhudumia magari 181,492.

Mkurugenzi huyo amesema, kwa kazi mkubwa ambayo watumishi wa TPA wameifanya,”wanahitaji kupongezwa kwani wamepokea na kupakia tani 41,000 za shaba ambapo hawajawahi kufanya huko nyuma.”

Aidha, hawa wafanyakazi kwa mwezi mmoja wa Novemba 2021 wamehudumia meli 71 na meli yenye uzito 4,9500 jambo ambalo ni kubwa halijawahi kufanyika.

Hamisi amesema, mapato kwa sasa kwa mwaka mmoja ni Sh.88 bilioni kwa mwezi na mpaka Februari 2022 jumla ya Sh.704 bilioni zilikuwa zimekusanywa ukilinganisha na Sh.590 bilioni iliyokusanywa kupindi kama hiki mwaka jana.

1 Comment

  • Hiyo shaba ya wazambia si inachukuliwa na wachina walioikamata Zambia. Makanikia tunauza kwa miaka mingapi?
    Tani 1900 za dhahabu wachina walipata wapi kama siyo kwetu?
    Msiiuze Tanzania yetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!