August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe: Tuna hofu kubwa

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

TUNA hofu kubwa ya kutotendewa haki ndani ya nchi. Ni kauli ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anaandika Mwandishi Wetu.

Kiongozi huyo wa upinzani anasema kuwa, upinzani una hofu kwa viongozi wake kuanzia ngazi ya taifa, wabunge, madiwani, vijiji, mitaa na vitongoji kutokana na wanavyotendewa na Serikali ya Rais John Magufuli.

Akiwa mjini Shinyanga kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho, Kanda ya Serengeti (Shinyanga, Mara na Simiyu) Mbowe amesema, nchi inapita katika kipindi kigumu.

Viongozi hao wamemaliza ziara ya Kanda ya Ziwa Victoria na Serengeti iliyolenga kuweka viongozi wapya watakaoendelea kukiongoza chama hicho mpaka kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Kutokana na hali ilivyo ndani ya nchi Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai, Kilimanjaro amesema kuwa, watu wameanza kujiona hawapo salama na kwamba, kila mmoja ana hofu na kitu fulani.

“Kuna watu wana hofu na njaa, kuna watu wana hofu na usalama wao, kuna watu wana hofu na uchumi. Sisi kama chama tuna hofu na usalama wetu, tuna hofu ya kutotendewa haki,” amesema Mbowe.

Ameeleza kuwa, namna viongozi wa upinzani wanavyofunguliwa kesi na hata kuhukumiwa kunazidisha hofu ya usalama wao na kwamba, namna mahakama zinavyotoa hukumu zinastaajabisha.

Amesema kuwa, Rais Magufuli amekuwa akitoa kauli za kuogofya na kwamba, si mpatanishi pale panapotokea sintofahamu na si mtu wa kutoa moyo tena Watanzania.

error: Content is protected !!