Sunday , 30 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makamba: Tulifunga milango matokeo tuliyaona
Habari za SiasaTangulizi

Makamba: Tulifunga milango matokeo tuliyaona

January Makamba
Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema hakuna mjadala kuhusu muelekeo wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwamba safari zake za nje, zina uhusiano mkubwa na maendeleo ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Aidha, amesema Watanzania ni mashahidi kuwa kuna wakati Tanzania ilijaribu kufunga milango ya ushirikiano na nchi za nje, na matokeo yake kwenye sekta ya uwekezaji, biashara na hata sifa na heshima ya Tanzania ikashuka.

Makamba ametoa kauli hiyo leo Alhamisi jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia ziara ya Rais Samia nchini Korea ambayo imewezesha upatikanaji wa mkopo wa masharti nafuu wa dola za Marekani 2.5 bilioni sawa na Sh 6.5 trilioni, kwa ajili ya miradi ya miundombinu.

Amesema kwa mujibu wa sera mambo ya nje ya mwaka 2001, inaitaka Tanzania kuchangamana kimataifa ili kutimiza malengo ya kimaendeleo.

Amesema katika misingi saba ya sera hiyo, msingi namba tano ni ushirikiano kimataifa wa maendeleo.

“Dunia ya sasa ni ya ushindani lakini pia ni ya ushirikiano, nchi zinashindana kupata masoko na maarifa katika maendeleo. Pia kuna changamoto za kidunia zinahitaji ushirikiano mfano mabadiliko ya tabia nchi.

“Kwa maana hiyo maarifa ya viongozi lazima yaguse ushirikiano na ushindani na katika kupata yote lazima kutafuta washirika ili kuhimili ushindani na kujenga uwezo na kutimiza malengo ya maendeleo.

“Hivyo kwa dunia ya sasa hamna namna ya kukaa ndani ya mipaka yako bila kutoka bila kuzungumza na dunia ukaamini utatimiza malengo yako, haitapata kutokea,” amesema.

Amesema Watanzania hujisifu tangu zamani kwamba nchi inaheshimika duniani kuliko uwezo wa kiuchumi na kijeshi lakini sifa hiyo haijaja kwa ajali bali imejengwa kwa viongozi wake tangu awamu ya kwanza kushirikiana na dunia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Tanzania yakubali kukutana na mabalozi 9 kutatua changamoto za kikodi

Spread the loveSerikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na...

error: Content is protected !!