Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mahakama: Makonda atangazwe gazetini, nyumbani kwao
Habari MchanganyikoTangulizi

Mahakama: Makonda atangazwe gazetini, nyumbani kwao

Paul Makonda
Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni leo Jumanne tarehe 8 Februari 2022, imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Anaripoti Mwandishi Wetu,  Dar es Salaam … (endelea).

Lengo ni ili kumwezesha Makonda kupata taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari mwandamizi, Saed Kubenea.

Kubenea amefungua maombi ya kufungua kesi ya jinai dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Makonda mwenyewe.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu, Aron Lyamuya ambaye ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 2 Machi 2022.

Ametoa uamuzi huo baada ya mawakili wa Kubenea, Nyaronyo Kicheere na Hekima Mwasipu kuiomba mahakama kutoa samasi ya kumtangaza kwani jitihada za kumpata Makonda ili kupatiwa wito wa kufika mahakamani kugonga mwamba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

error: Content is protected !!