Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo GSM yajiondoa udhamini Ligi Kuu
Michezo

GSM yajiondoa udhamini Ligi Kuu

Ghalib Said Mohammed
Spread the love

 

KAMPUNI ya GSM imejiondoa kwenye udhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kufuatia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi kushindwa kutimiza makubaliano ya kimkataba waliokubaliana pande zote mbili. Anaripoti Mwandishi Wetu

Uamuzi wa kampuni hiyo kujiondoa kwenye nafasi hiyo ya uamuzi mwenza, ulitangazwa jana Februari 7, mwaka huu na mbnele ya waandishi wa habari na Allan Chonjo, Afisa Biashara Mkuu wa kampuni hiyo.

Afisa huyo alisema kuwa kampuni hiyo ilishawishika sana na Tff na bodi ya Ligi kulidhia kuwa mdhamini mwenza wa Ligi hiyo, kwa nia ya kukuza sekta ya michezo nchini lakini mambo yalikuwa tofauti.

“Haya hayajawa mamuzi rahisi kama kampuni kwani tunatambau ya kuwa vipo baadhi ya klabu za mpira wa miguu vitakavyoumizwa pamoja na wadau mbalimbali na hatua hii haikuwa dhamira yetu kufikia huku”Alisema Afisa huyo

Novemba 23, 2021 kampuni ya Gsm iliingia mkataba na Tff ambaye alikuwa anawakilisha klabu zote 16 za zinazoshiriki Ligi Kuu msimu huu, wenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.1 katika kipindi cha miaka miwili.

Mara baada ya kusaini kwa mkataba huo, klabu ya soka ya Simba iliandika barua kwenda kwa Bodi ya Ligi, kutaka ufafanuzi wa mkataba ambao Tff uliingia dhidi ya kampuni ya Gsm ya udhamini mwenza wa Ligi Kuu.

Katika barua hiyo Simba ilitaka ufafanuzi ma masuala mbalimbali kabla ya utekelezaji wa mkataba huo ikiwemo kuvaa Nembo ya mdhamini huyo kwenye jezi yao huku wakidai ni kinyume na kanuni.

Aidha hoja nyingine za Simba katika barua yao hiyo ni kuwepo kwa mgongano wa maslai kati ya kampuni hiyo ya Gsm na klabu ya Yanga ambao ni wafadhili wao katika mambo mbalimbali.

Barua ya Simba ilieleza kuwa wanashindwa kutofautisha maofisa wanaofanya kazi Gsm na wanaofanya kazi na Yanga, kwa kuwa kaimu Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga Mhandisi Hersi Said ndio huyo huyo aliwakilisha Gsm katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika tarehe 23, Novemba 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!