May 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lissu ajigamba ‘sipoi’

Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema licha ya Ofisi ya Kanda ya Kaskazini kuchomwa moto, ratiba yake ya leo haibadiliki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Taarifa kutoka Arusha zinaeleza, usiku wa kuamkia leo tarehe 14 Agosti 2020, Ofisi za Chadema kanda hiyo zimeshambuliwa na kuteketea kwa moto.

Jeshi la Polisi jijini Arusha limeeleza kuendelea na uchunguzi na kisha kutoa taarifa ya nini kilichotokea.

Kwenye ukurasa wake wa twitter, Lissu ameandika kwamba, tayari ameingia kwenye jiji hilo kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili kukamilisha utaratibu wa Tume ya Uchaguzi (NEC) ya kupata wadhamini wa urais kutoka kila mkoa.

Hata hivo ameeleza, pamoja na tukio hilo baya kutokea akiwa ndio ameingia kwenye mkoa huo, tukio la shambulizi kwenye ofisi hizo halitikisi kile alichokusudia kufanya leo.

“Ofisi zetu za chama za Kanda ya Kaskazini zilizopo Arusha zimeshambuliwa na kuharibiwa wakati nikiingia Arusha. Ratiba ya leo itabaki vile vile. Hakuna kiwango chochote cha hofu kinaweza kuzuia mabadiliko haya ya sunami Tanzania,” amesema.

error: Content is protected !!