Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko LHRC yalaani mauaji ya kinyama Tabora
Habari Mchanganyiko

LHRC yalaani mauaji ya kinyama Tabora

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga
Spread the love

 

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), kimeiomba Serikali ya Tanzania, kuwachukulia hatua watu waliohusika katika tukio la mauaji ya mtoto Nyanzobhe Mwandu (4), lililotokea tarehe 16 Juni 2021, mkoani Tabora. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ombi hilo lilitolewa jana Jumatatu, tarehe 21 Juni 2021 na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga lipozungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo linatajwa kutokea katika operesheni iliyofanywa na Askari Polisi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Wanyamapori (TAWA),  kwa lengo la kuondoa wananchi wanaodaiwa kuvamia eneo la hifadhi ya Kijiji ya Ngitiri mkoani Tabora.

Askari hao wanadaiwa kuchoma baadhi ya nyumba za wananchi hao, hivyo kusababisha mtoto aliyekuwepo kwenye moja ya nyumba hizo kuteketea kwa moto.

“Tukiwa kama wadau tunalaani tukio la kuchomwa moto nyumba ambayo ndani yake kulikuwa na mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne, ajulikanae kwa jina la Nyanzobhe Mwandu,” amesema Henga.

Henga ameiomba Serikali, imemchukulia hatua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Abel Busalama Yeji, anayedaiwa kutoa amri iliyosababisha nyumba hizo zichomwe moto.

“Kitendo kilichofanywa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, kimepelekea kukatiza uhai wa mtoto, huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu. LHRC kinatoa raia kwa Serikali kuhakikisha aliyekuwa Yeji anawajibika,  kutokana na kitendo cha kukatisha maisha ya mtoto kilichosababishwa na amri yake kwa Askari wa TAWA na askari wa Polisi wa Kituo cha Igagala,” amesema Henga.

Pia, Henga amemuomba  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu na Waziri wa Maliasili na utalii, Dk. Damas Ndumbaro,  kufanya ziara vijiji vyite vilivyopo kwenye kata ya Usinge, kwa ajili ya  kusikiliza kero za wananchi.

MwanaHALISI Online ilimtafuta kwa simu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Tabora, Safia Jongo, kwa ajili ya kupata taarifa zaidi juu ya tukio hilo, ambapo alisema tume imeundwa kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo.

Kamanda Jongo alisema, Jeshi la Polisi linafanya mahojiano na baadhi ya wananchi na Askari Polisi wa TAWA, na kwamba zoezi hilo likikamilika watatoa taarifa kwa umma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

Habari Mchanganyiko

Uholanzi wampongeza Rais Samia kuimarisha vyombo vya habari, demokrasia

Spread the love  UBALOZI wa Uholanzi nchini Tanzania, umempongeza Rais Samia Suluhu...

error: Content is protected !!