May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bajeti 2021/22 kupitishwa? Spika Ndugai atoa onyo

Job Ndugai Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania

Spread the love

Bajeti 2021/22 kupitishwa? Spika Ndugai atoa onyoMJADALA wa Bajeti ya Serikali ya Tanzania kwa mwaka 2021/22 ya Sh.36.3 Trilioni, unahitimishwa leo Jumanne, tarehe 22 Juni 2021, bungeni jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Tayari Spika wa Bunge, Job Ndugai ametoa onyo kwa mbunge ambaye hatopiga kura kuipitisha bajeti hiyo huku akiwa hana ruhusa yake, litakalomkuta “ni la kwakwe mwenyewe.”

Bajeti hiyo, iliwasilishwa bungeni hapo, Alhamisi tarehe 10 Juni 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba.

Baada ya kuiwasilisha, wabunge walipata fursa ya kuijadili kuanzia tarehe 14 Juni 2021.

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Leo Jumanne asubuhi, kabla ya kipindi cha maswali na majibu kuanza, Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai amewashukuru wabunge kwa kuijadili vyema bajeti hiyo, ikiwemo wenyeviti wa Bunge na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kwa kuongoza Bunge.

“Leo ni siku ya uamuzi na kwa mbunge ambaye hayupo hapa na hatapiga kura yake, hilo ni la kwake mwenyewe,” amesema Spika Ndugai

error: Content is protected !!