Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Korosho pasua kichwa, CUF wataka bodi ichunguzwe
Habari Mchanganyiko

Korosho pasua kichwa, CUF wataka bodi ichunguzwe

Zao la Korosho
Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeiomba Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kufanya uchunguzi dhidi ya Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), kuhusu tuhuma za kusambaza pembejeo za kughushi ‘feki’, kitendo kilichoathri uzalishaji wa zao hilo katika mikoa ya Kusini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo Jumanne, tarehe 25 Oktoba 2022, jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa CUF, Maftaha Nachuma, ametaka uchunguzi huo ufanyike ili kuwachukulia hatua watu waliohusika katika sakata hilo, kwa kuwa wanamhuju Rais Samia Suluhu Hassan.

Makamu Mwenyekiti huyo wa CUF-Bara, amesema wakulima waliofikiwa na pembejeo hizo, maua ya mikorosho yao yamekauka na kushindwa kufanya uzalishaji. Wilaya zinazodaiwa kuathirika na changamoto hiyo ni Newala, Nanyamba, Tandahimba, Masasiu, Tunduru, Kibiti, Rufiji na mingine.

“Tulikuwa tunaimani na jitihada za Rais Samia kuwaondoa Watanzania katika umasikini lakini hali imebadilika kwa hili lililojitokeza kwa wakulima wa korosho, CUF kinaitaka Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwachukulia hatua wahusika wote walioagiz dawa fake za mikorosho pamoja na kuwalipia fidia wakulima wote waliopatwa na kadhia hii,” amesema Nachuma.

Katika hatua nyingine, Nachuma amedai Bodi ya Korosho imeshindwa kusimamia bei za zao hilo katika minada iliyofanyika kuanzia Oktoba, 2022, na kupelekea kuporomoka hadi kufikia Sh. 1,714 kwa kilo katika baadhi ya maeneo.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Kaimu Mkurugenzi wa CBT, Francis Alfred, amejibu akisema “watu wanaojua dawa feki au sio feki ni mamlaka ya afya ya mimea ndiyo wanajua hayo sio bodi. Sisi hatuna hizo taarifa labda aliyeambiwa athibitishe lakini sisi hatuna taarifa kutoka kwa wakulima.”

Kuhusu wakulima kulalamikia bei ya korosho, amesema “wakulima kukataa bei ni jambo la kawaida, mnunuzi anatoa bei yake na mkulima ana haki ya kuikubali au kuikataa na hii haijaanza mwaka huu hata mwaka jana wakulima walikataa kuuza sababu hayo ni makubaliano kati ya mkulima na mteja.”

Meneja Mkuu wa Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Korosho wilaya ya Tandahimba na Newala, mkoani Mtwara (TANECU), Mohamed Mwinguku, alipoulizwa kuhusu suala hilo amesema “hilo siwezi kulizungumzia sasa hivi sababu sina ushahidi hakuna mkulima aliyenilalamikia. Labda uwaulize wakulima wenyewe.”

Mkulima wa Korosho, wilayani Tandahimba, Mkoa wa Mtwara, Karim Chipola, alipoulizwa kama uzalishaji wa zao hilo umeshuka kutokana na baadhi ya wakulima kupewa pembejeo feki, amejibu akisema taarifa hizo si za kweli kwani kwa upande wake hajasikia wakulima wenzake wakilalamika kuhusu suala hilo.

“Unaposema uzalishaji umeshuka unamaanisha nini? Sababu sasa hivi tunaendelea na mavuno maana mtu anaposema uzalishaji umepungua yaani ufikie kiwango cha mwisho cha uzalishaji kwa mavuno kujua mwaka jana zilivunwa tani kadhaa na mwaka huu zimevunwa tani kadhaa,”

“Mimi binafsi mwaka jana nilipata na mpaka sasa kimeongezeka na bado naendelea kuvuna, mwaka jana nilipata tani 30, lakini hadi sasa nimepata tani 60 na naendelea kuvuna,” amesema Chipola na kuongeza:

“Ukija nyumbani kwangu nitakuonyesha nina magunia 500 ya korosho. Serikali haiwezi fanya vitu vya ovyo kusambaza pembejeo feki sababu kuna watu wanasimamia ubora, mfano mwaka jana salfa zilikuwa chini ya kiwango hazikugawiwa. ndugu zetu wanaongea bila kuthibitisha kwa wakulima ilimradi kupata stori.”

Tuhuma za wakulima wa korosho kupewa pembejeo feki ziliwahi kuibuliwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka, alipofanya ziara ya katika mikoa ya kusini, Juni 2022, ambapo alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mtwara, kumchukulia hatua mfanyabiashara anayeuza pembejeo feki.

Shaka alisema “kweli huyo mtru bado yupo mtaani , sijui kwa sababu ana nguvu ya fedha mimi nashangaa vyombo vya ulinzi na usalama havijamtia mkononi bado na anasambaa ndani ya mkoa huu wa Mtwara.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!