Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara zamlilia Mkapa
Michezo

Klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara zamlilia Mkapa

Spread the love

BAADHI ya klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara zimetuma salamau za rambirambi kufuatia kifo cha Aliyekuwa Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamini William Mkapa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kifo cha Rais huyo mstaafu kimetokea usiku wa kuamkia leo kwa taarifa hiyo kutangazwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, John Magufuli kwa watanzania na kutangaza maombolezo ya siku saba.

Baadhi ya klabu zilizotuma salamu za pole ni pamoja na Namungo, Yanga, Azam FC pamoja na Simba kupitia kuraza zao kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa upande wa klabu ya Yanga wao walituma salamu hizo kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa inastagram kwa kutoa pole kwa familia juu msiba huo.

“Young Africa Sports Club tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Benjamini William Mkapa,” ilieleza taarifa hiyo.

Aidha kwa upande wa klabu ya Azam FC kupitia kurasa yao ya mtandao wa kijamii wa Twitter iliyoeleza masikitiko yao juu ya kifo hicho.

“Pumzika kwa amani, Rais wetu mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Benjamini William Mkapa,” ilieleza taarifa hiyo kutoa Azam FC.

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya Simba, kupitia kurasa zao za mitandao ya Twitter na Instagram walitoa taarifa kuonesha uongozi wa klabu hiyo ulivyo sikitishwa na msiba huo.

“Uongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini Mkapa, Simba tunatoa pole kwa familia, ndugu na watanzania wote.”

Aidha klabu ya Namungo nayo haukuwa nyuma kuonesha masikitiko yao juu ya kifo cha raisi huyo wa awamu ya tatu kwa kuweka picha yake yenye maneno ya Pumzika kwa amani.

Mkapa atakumbukwa sana kwenye sector ya michezo kwa kujenga Uwanja wa michezo wa kisasa wenye uliopewa jina la Uwanja wa Taifa wenye kubeba idadi ya watazamaji 60000 na kuwa moja ya viwanja bora barani Afrika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!